Namna mpya ya kupima saratani kwa kutumia vipimo vya mkojo

Utafiti umebainisha kuwa wanawake wanaonekana kuwa na hofu au kuona aibu kwenda kufanya vipimo vya saratani hivyo badala yake uamua kutoa sampuli ya mkojo ili kupimwa saratani ya uzazi.

Jaribio la vipimo hivyo vya mkojo vinaweza kupima virusi vya magonjwa ya zinaa yanayofahamika kama HPV ambavyo vinaweza kupelekea mtu kuwa hatarini kupata saratani ya shingo ya uzazi.

Kuna haja ya kuwepo kwa majaribio mengine makubwa lakini wataalamu wanasema vipimo hivyo ambavyo vinaruhusu mtu kujipima mwenyewe inaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwa wanawake.

Idadi ya watu ambao wanafanya vipimo vya saratani ni ndogo kuliko nchini Uingereza.

Vipimo vya saratani vinazuia asilimia sabini na tano ya saratani ya uzazi hivyo vipimo hivyo vinaweza kuwa sio rafiki kwa wengi lakini ni muhimu.

Vipimo vya saratani vinaweza kutoa majibu mapema kabla ya saratani haijaanza kukua.

Watu mashuhuri na wapiga kampeni wamejaribu kuwahamasisha wanawake wengi zaidi kufanya vipimo hivyo lakini sasa wanaangalia namna nyingine ya kuboresha vipimo vya saratani.

Baadhi ya tafiti zilizofanywa tayari zilikuwa zinauliza wanawae kujaribu kujipima wenyewe nyumbani.

Kwa sasa hakuna watafiti ambao wamethibitisha kuwa kupima mkojo inaweza kuwa njia mbadala ya kupima saratani.

Kati ya wanawake 104 ambao walifanyiwa jaribio la vipimo vya mkono katika klinini moja iliweza kugundua kuwa kipimo hicho cha mkojo kinafanya kazi sawa na kipimo cha saratani kinachofanywa hospitalini katika kubaini haari kubwa ya HPV.

Kampeni za kuhamasisha wanawake kufanya vipimo vya saratani vimesaidia.

Aidha kwa wanawake ambao walifanyiwa ukeketaji au wanawake ambao walikutana na unyanyasaji wa kingono unaweza ukaleta changamoto.

Hata hivyo wanawake bado wanaendelea kufanya vipimo hivyo vinavyojulikana kama vipimo vya kuokoa maisha.