Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mifupa thabiti, furaha na usingizi mwororo; manufaa ya mwangaza maishani mwako
Iwapo una siku ndefu au fupi kutokana na sehemu yoyote ile unayosihi duniani, mwangaza unakuathiri.
Kwa wanaoishi katika maenoe ya baridi ambapo usiku unakuwa mrefu na hata katika maeneo yetu ya kusini mwa jangwa la sahara ambapo kuna baraka tele za jua na mwanga - kupokea miale ya mwanga wa jua hilo ni muhimu kwa afya yetu.
Wengi wetu huhisi kuwa wachangamfu na wenye furaha nyingi kila jua linapochomoza - na kinyume cha hicho kunaponyesha mvua au mawingu yanapotanda na kiza kuingia.
Na kuna sababu kwanini tunahisi hivyo wakati mwangaza unaimarisha mifupa yetu mwilini sawa na ubongo.
Haya ndio manufaa yake...
1. Mwangaza unaturuhusu tulale na tuamke
Mojawapo ya kazi kuu ya kibayaolojia inayotokana na mwangaza ni uwezo wa kuuambia mwili kulala - unaruhusu mwili wetu ufahamu kwamba mfumo unashinikiza mtu kuwa macho unafanya kazi.
Sawana hilo, jua linapotua na kiza kinapoingia, miili yetu huanza kusambaza kemikali ya melatonin, inayotusaidia kupata usingizi.
Ndege kadhaa sasa zinatumia taa za ndani ya ndege kusaidia kukabiliana na mchoko wa safari kwa jina jigine jet lag, kwa kuwasha taa zenye mwanga mkubwa wakati wa kuabiri, ta za wastani wakati wa kula na taa zenye mwanga mdogo kuwasaidia abiria kupata lepe la usingizi.
2. Mwangaza unakusaidia kukabiliana na ukosefu wa usingizi
Sasa tunafahamu kwamba taa ya samawati ianyotoka kwenye mwangaza wa kompyuta zetu, simu na tabiti zinatuzuia kuwa na homoni za usingizi zinazotusaidia kulala.
Muogozo mpya kutoka idara tofauti za afya - zinaeleza kwamba tunasahili kutotazama simu,televisheni na vifaa vingine vya teknolojia muda mfupi kabla ya kulala , na vifaa hivyo vinastahili kuwekwa nje ya vyumba vya kulala.
Matthew Walker - mwansayansi wa ubongo anayfanya utafiti kuhusu usingizi - anakubaliana na hilo na anasema kwamba "mwanagza wa mchana ni muhimu katika kuratibu mkonodo wa usingizi kila siku".
3. Mwangaza unaathiri hisia zako
Dozi ya mwangaza wa kila siku inaweza kukusaidia sio tu katika usingizi - lakini pia inaathiri ubongo wako kwa kuleta hisia za furaha.
Mwili unaptambua kuna mwangaza wa jua, ujumbe naofika kwenye ubongo kupitia mishipa ya macho, viwango vya kemikali ya serotonin huongezeka mwilini.
Kwa ukubwa zaidi viwango vya mwangaza huo huzuiwa - kama kwa wafanyakazi wa zamu - ambao utawakuta wanakabiliana na msongo wa mawazo.
Kuna taizo moja la akili ambalo linahusiana moja kwa moja na kutokuwepo wa mwangaza katika msimu wa baridi na kiza kingi: Seasonal Affective Disorder (SAD).
Waathiriwa wa SAD mara nyingi huwa na dalili za msongo wa mawazo, zinazojitokeza siku inapokuwa fupi na hali hiyo hufifia unapoingia msimu wa machipuko.
4. Mwangaza wa jua unaimarisha mifupa mwilini
Tunahitaji vitamin D ili miili yetu iweze kunyonya au kupokea calcium na phosphate kutoka kwenye vyakula tunavyokula - madini yalio muhimu ili kuwa na mifupa yenye afya, meno na hata misuli.
Ukoseu wa vitamin D unaweza kusababisha mifupa kuwa laini na ilio dhoofu na pia kupata matataizo ya mifupa.
Na kwa bahati nzuri na kwa urahisi vitamin D hupatikana katika jua.
Miili yetu hupata vitamin D wakati jua linapotupiga kwenye ngozi.
Lakini pia, jua jingi sana ni hatari - kwa hiyo ni muhimu kupaka mafuta ya kuzuia miale ya jua kupiga sana mwilini wakati wa joto jingi mchana.