Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Takwimu: Miti asilia inaongoza kwa kupotea kwa kiwango kikubwa zaidi duniani
Ni karibu hekta milioni 12 ya misitu katika dunia ya kitropiki ilipotea mwaka 2018, ambapo ni sawa na kupoteza viwanja 30 vya mpira wa miguu kwa dakika.
Wakati ripoti hii ikiwasilisha kupungua kwa misitu kwa mwaka 2016 na 2017, ingawa bado upoteaji wa misitu ulikuwa umeanza tangu mwaka 2001.
Na huku wasiwasi mkubwa ni kwamba uharibifu wa misifu bado unaendelea.
Kwa nini takwimu hizi ni muhimu?
Ripoti ya 'Global Forest watch' inaonyesha picha ya namna ambavyo misitu mikubwa ya kitropiki inavyopitia wakati mgumu duniani kuanzia eneo la Amazon huko Amerika ya kusini, Afrika ya kati na kaskazini mpaka Indonesia.
Misitu ya Amazon ni eneo la makazi ya watu takribani milioni ishirini.
Miongoni mwa watu hao ,makabila mbalimbali wanaishi katika eneo lililotengwa.
Pamoja na kutoa chakula na makazi, miti katika eneo hili ni muhimu duniani ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mamilioni ya hekta za misitu imekuwa ikipotea katika karne ya hivi karibuni kutokana na shughuli za kibiashara na kilimo.
Takwimu za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa kuna utofauti katika upungufu mkubwa wa misitu kwa miaka miwili iliyopita huku miti mingi ikiwa imepotea kutokana na moto.
Hata hivyo waliohusika na utafiti wanasema kuwa habari njema hii ndio ilikuwa inatazamiwa.
"Hali hii inaleta shauku ya kuanza kusheherekea mwaka wa pili wa kupungua kwa miti tangu jitihada zilipoanza mwaka 2016," alisema Frances Seymour kutoka Taasisi ya rasilimali duniani ambayo inaongoza Global Forest Watch.
"Lakini ukiangalia miaka 18 nyuma, ni wazi kuwa bado tatizo ni kubwa na hatuko karibu kushinda vita hii."
Misitu ya msingi ni ipi na kwa nini ni muhimu?
Msitu ya msingi ni ile inayopatikana kiasilia na huwa haipandwi na binadamu au kuhudumiwa kwa namna yoyote.
Muda mwingine huwa tunaitambua kama misitu ya zamani , maana miti hiyo ya asili ina uwezo wa kukaa miaka mingi, mamia au hata maelfu.
Miti hiyo ambayo huwa makazi ya wanyama kama chui ,sokwe na wengine wengi.
Misitu hii ya zamani huwa inasaidia sana kutunza hewa ukaa, ndio maana upoteaji wa hekta milioni 3.6 mwaka 2018 ulitiliwa maanani.
Kwa kila hekta inayopotea katika msitu, tuko hatua moja karibu kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Je, ni misitu ya Amazon tu ndio imeathirika?
Hapana!
Mwaka 2002, Brazil na Indonesia iliweza kupoteza misitu asilia asilimia sabini na moja.
Mwaka 2018 ,nchi mbili zilipoteza asilimia arobaini na sita.
Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ni nchi ya pili duniani kwa kupoteza misitu huku Colombia, Bolivia na Peru pia kuna ongezeko kubwa la kupotea kwa misitu asilia.
Madagasca ilipoteza asilimia mbili ya misitu asilia mwaka 2018.
Upoteaji wa miti hii unasababisha athari kubwa katika eneo husika", alisema Frances Seymour.
"Mamia ya watu uuwawa wanapojaribu kukataza wanaofanya uharibifu huo kuacha kwa sababu ya kulinda maslahi yao ya kibiashara na utajiri"
Nchi kama Ghana na Cote d'Ivoire zimepoteza eneo kubwa la msitu asilia,
Ghana imepoteza asilimia sitini huku Cote d'Ivoire ina athari ya kupotea kwa misitu ni asilimia 26.
Ongezeko hili haswa kwa Ghana , limesababishwa na wachimbaji wadogo wa madini na vilevile kukua kwa ukulima wa kakao.
Wanaofanya kampeni juu ya ongezeko la upunguaji wa misitu ilitoa ripoti muongozo 2017 kwa kampuni za chokoleti na kokoa, kusitisha ukataji wa misitu kutokana na mzunguko wa uzalishaji wa bidhaa zao.
Kulikuwa na habari njema katika jitihada hizo?
Cha kushangaza zaidi ni ndio.
Indonesia iliweza kufanikiwa kupunguza upoteaji wa misitu asilia mwaka 2018 kwa asilimia 40 tangu mwaka 2003.
Licha ya kuwa serikali imefanya jitihada kubwa kulinda eneo hilo lisiathirike na upoteaji wa misitu,