Mtoto mwenye wazazi watatu azaliwa

Chanzo cha picha, SPL
Madaktari wataalamu wa masuala ya uzazi nchini Ugiriki na Uhispania wamesema wamesema mtoto amezaliwa kutokana na wazazi watatu njia iliyotumika kukabiliana na tatizo la utasa.
Mtoto wa kiume alizaliwa akiwa na kilo 2.9 siku ya Jumanne.Mtoto na mama wanaelezwa kuwa na hali nzuri.
Madaktari wanasema wanaweka tukio hilo kwenye kumbukumbu za kihistoria ambayo itawasaidia wenza wasioweza kupata mtoto duniani.
Lakini wataalamu wanasema mchakato wa upatikanaji wa mtoto huyo umesababisha maswali mengi ya maadili ya kazi na usingefanyika.
Majaribio hayo ya upandikizaji yalihusisha mayai kutoka kwa mama, mbegu za kiume za baba na yai moja kwa mwanamke aliyejitolea.
Njia hii ni kwa ajili ya kuzisaidia familia zilizoathiriwa na maradhi ya kijenetiki, (Mitochondria) ambayo huambukiza kutoka ka mama kwenda kwa mtoto.
Ilijaribiwa mara moja kwa familia moja huko Jordan hatua iliyoleta mkanganyiko mkubwa.
Mitochondria ni vichumba vidogo ndani ya kila seli ya mwili vinavyobadilisha chakula kuwa nishati.

Umbo la Seli:
Nucleus (Kiini) : Vinasaba hushikiliwa hapo , hutusaidia katika kujifahamu jinsi tulivyo.
Mitochondria: huelezwa kuwa vyumba vya ndani ya Seli ambavyo husaidia Seli kufanya kazi.
Cytoplasm: Ni majimaji yenye kiini na vyumbavyumba vilivyo kwenye seli
Daktari Panagiotis Psathas,Rais wa Taasisi iitwayo Life mjini Athens, amesema ''Ndoto ya mwanamke ambaye hakuweza kupata haki yake ya kupata mtoto kwa kutumia jeni zake mwenyewe inakuwa na uhalisia.''
''Tunafurahi kutangaza kuwa sasa tuna uwezo wa kufanya ndoto za wanawake zitimie hasa wale ambao wamefanya upandikizaji (IVF) mara nyingi bila mafanikio au kwa wale wanaokabiliwa na maradhi ambayo yanawazuia kupata mtoto mwenye afya.''
Timu ya Ugiriki na kituo cha kiafya cha Uhispania ambacho kilitangaza kuwa wanawake 24 wanajitolea kwenye majaribio hayo na tayari viumbe vilivyopatikana baada ya kurutubishwa viko tayari kupandikizwa.
Mwezi Februari mwaka 2018, madaktari huko Newcastle ambao walianzisha teknolojia hii walipewa idhini kuunda watoto waliotokana na wazazi watatu nchini Uingereza.
Daktari Tim Child kutoka Chuo cha Oxford amesema ''athari za upandikizaji huo hazifahamiki, ingawa labda unaweza ukakubalika kama utatumika kutibu maradhi yanayomfanya mwanamke ashindwe kupata mtoto.''












