Mwanamke ajifungua mtoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi India

Chanzo cha picha, Galaxy Care Hospital
Meenakshi Valand ni mmoja kati ya watu wachache duniani ambao wamejaaliwa kupata watoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi.
Alikuwa na furaha isiyokuwa na kifani.
"Sikuweza kujizuia kulia baada ya kusikia sauti ya mwanangu akilia. Haya ni machozi ya furaha - Nimepoteza watoto sita katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita," aliiambia BBC.
Mama huyo wa miaka 28-alijifungua mwezi uliyopita nchini India baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi wa mamake mzazi.
Katika miaka tisa ya ndoa yake, Meenakshi alizaa watoto wawili waliofariki, alipoteza wengine wanne katika uja uzito, hatua iliyomsababisha kukatika kwa mfuko wake wa uzazi.
Hali hiyo inajulikana kama Ashermans syndrome.
Lakini hakukata tamaa. "Nilitaka kuwa na mtoto wangu mwenyewe. Sikutaka kutumia mbinu nyingine yoyote."
Kwa mujibu wa jarida la kimataifa la utafiti wa kisayansi, 15% ya watu hawana uwezo wa kuzaa na 3 kati ya 5% ya visa hivi husababishwa na matatizo ya mfuko wa uzazi.

Chanzo cha picha, Galaxy Care Hospital
Alimtembelea Dkt Shailesh Putambekar, mtaalamu wa upasuaji na upandikizaji wa mfuko wa uzazi katika hospitali ya Galaxy Care mjini Pune.
Wakati huo mama yake Sushila Ben alikuwa amejitolea kumpatia mfuko wake wa uzazi ili kumuezesha kupata mtoto.
Upandikizaji huo ulifanywa na kundi la wataalam 12 mwezi Mei mwaka 2017 na ulifanikiwa.
Lakini Januari mwaka huu alikabiliwa na changamoto nyingine baada ya hatua ya kuhamisha kijusi kukwama.
Hata hivyo utaratibu huo ulifanywa tena mwezi Aprili.
Wiki 20 baadae mwanawe Radha alizaliwa kabla ya kufikisha wakati wa kuzaliwa akiwa na kilo 1.45.
Dkt Putambekar alisema , "Meenakshi alianza kupata matatizo mengine ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu hali ambayo ilitulazimu kumfanyia upasuaji wa dharura ili kumuokoa mama na mtoto.
Mtoto alizaliwa salama lakini kabla ya wakati na alikuwa na kilo 1.45 ''Lakini anaendelea vizuri hana neno''
Huu ilikuwa mfumu wa kwanza wa kuzalisha ambao ni wa 12 kote duniani.
Upandikizaji wa mfuko wa uzazi enzi hizi:

Chanzo cha picha, Getty Images
Upandikizaji wa mfuko wa uzazi umefanywa katika mataifa 10 ikiewemo: Sweden, Saudi Arabia, Uturuki, Marakani, Uchina na Jamhuri ya Czech, Brazil, Ujerumani, Serbia na India.
- 2014 - Mwanamke kutoka mji wa Gothenburg, nchini Sweden alijifungua mtoto wa kiume kupitia utaratibu wa kupandikizwa mfuko wa uzazi.
- Mwanamke huyo wa miaka 36 alipata mhisani wa miaka 60 aliyempatia kizazi.
- 2017 - Mwanamke katika mji wa Dallas, Texas, alizaa mtoto kupitia mfumo wa upandikizaji wa mfuko uzazi nchini Marekani.
- 2018 - Mwanamke alifanikiwa kujifungua mtoto wa kisichana kupitia upandikizaji wa mfuko wa uzazi kwa mara ya kwanza nchini India.
- Watoto 12 wamezaliwa kupitia mfumo huo nane kati ya watoto hao wamezaliwa nchini Sweden.
- Ni mwanamke mmoja tu kati ya 12 aliyepandikizwa kizazi cha mtu aliyekufa.
Mfumo huu unafanya kazi vipi?
Wakati wa upandikizaji wa mfuko wa uzazi mfumo wa neva haupandikizwi kwa hivyo mwanamke hapati uchungu wakati wa kujifungua mtoto.
Mfumo huu maalum ulipoanza ulikuwa ukichukua hadi saa 13 kufanywa. "Lakini sasa upandikizaji wa mfuko wa uzazi unachukua saa sita anasema Dkt Shailesh Puntambekar.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa mujibu wa kundi la wataalamu katika hospitali ya Galaxy Care, mfumo wa upandikizaji wa mfuko wa uzazi unagharimu karibu dola 11000.
Lakini katika kesi ya Meenakshi Wayanad ambayo ni ya kwanza na aina yake nchini India, hakutakiwa kulipa chochote.
Alipewa dawa za kudhibiti mfumo wa kinga mwilini ili kuzuia mfuko mpya wa uzazi kukataliwa.
Mwaka mmoja baada ya upandikizaji, madkatari waliamua kukipandikiza kijusi kilichokuwa kimegandishwa.
Wanasema upandikizaji unadhaniwa kuwa salama kwa mama na mtoto licha ya kutumiwa kwa dawa inayofahamika kama (immuno-suppressants) pamoja na kuhusishwa kwa upasuaji wa aina tofauti.
Nchini India pekee karibu wanawake 600 wamewekwa katika orodha ya watu wanaotaka kufanyika upandikizaji wa kizazi kipya

Chanzo cha picha, Getty Images
Uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na utaratibu wa kupandikiza mfuko wa uzazi umebaini kuwa utaratibu huo umepata ufanisi mkubwa lakini unahitaji majaribio ya kliniki ya kudhibiti kisaikolojia na ukaguzi katika ngazi kadhaa.
Wakichangia katika jarida la kimataifa la masuala ya uzazi kundi la madaktari kutoka Japan limesema huku utaratibu wa kupandikiza mfuko wa uzazi ukisifiwa kwa kuwapa faraja wanawake waliyo na tatizo la mfuko wa uzazi bado utaratibu huo unaendelea kufanyiwa majaribio.
Matumaini ndiyo kitu Meenakshi alikuwa akijipatia: "Nimeteseka sana lakini sasa nina furaha kupita maelezo."














