Waziri Malusi Gigaba, amejiuzulu Afrika kusini baada ya kuanikwa mitandaoni akijichua

Afrika Kusini waziri na mkanda wa ngono

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waziri wa mambo ya ndani nchini Afrika Kusini , Malusi Gigaba,

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Afrika Kusini, Malusi Gigaba, amejiuzulu nafasi yake hiyo wiki mbili baada ya kipande cha video inayomuonesha akijichua kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa mapana nchini humo.

Taarifa kutoka ofisi ya rais ilisema Bw Gigaba ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama tawala African National Congress-ANC , kujivua nafasi zao kwa heshima ya nchi yake na harakati zinazomhusu.

Bwana Gigaba amevishutumu vyombo vya usalama nchini Afrika Kusini kwa kudukua simu yake na kuachilia kipande cha vido chenye urefu wa sekunde kumi na tatu , ambayo alijitetea kuwa alimrekodia mkewe.

Gigaba ana umri wa miaka arobaini na saba , miaka ya hivi karibuni amejikuta katika mkanganyo wa mambo kutokana na kutumia madaraka yake vibaya katika huduma mbalimbali na kuisaidia familia ya wafanyabiashara ya Gupta yenye utata.

Wafanya biashara hao wenye asili ya nchini India wanahusishwa sana na kashfa kadhaa za rushwa chini ya utawala wa Rais Jacob Zuma.katika kila hali ikiwa ni pamoja na Bwana Gigaba, wamekana makosa yoyote.

mkanda wa ngono wa waziri wa mambo ya ndani nchini Afrika Kusini

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Mmoja wa wafanya biashara kutoka familia ya Gupta, aitwaye Sanjeev Gupta ambaye ni mfanya biashara mkubwa katika sekta ya chuma nchini Uingereza.

Turejee kwenye hoja ya msingi, ya waziri wa mambo ya ndani nchini Afrika Kusini kuonekana mitandaoni akijichua wengi walihoji juu ya Gigaba kuendelea kushikilia ofisi, wakisema amepoteza sifa yake na kwamba taswira yake ulimwenguni na nchini humo imeharibiwa.

Wiki za hivi karibuni, swali liliulizwa kwa upana, kwanza juu ya uamuzi wa Mahakama ya Katiba ambayo imesisitiza awali kwamba alisema uongo chini ya kiapo wakati wa kutoa ushahidi kuhusu mkataba wa serikali.

Hali hiyo imearifiwa kutokana na mapendekezo ya muendesha mashtaka kuwa Gigaba akikutwa na hatia ataadhibiwa kwa uvunjaji wa maadili.

Vyama vya upinzani vimekuwa vikimshinikiza raisi Cyril Ramaphosa kumtimua kazi waziri huyo, na kwamba wamepokea kwa mikono miwili kujiuzulu kwake.