Mwendesha baisikeli asimulia jinsi mbwa koko alivyobadilisha mtazamo wake maishani

Illustration of Ishbel's route and Lucy

Mwendesha baisikali Ishbel Holmes ameshiriki mashindano mengi na kusafiri maeneo tofauti duniani, lakini amepitia maisha magumu alipokua mtoto mdogo.

Alifukuzwa nyumbani na mama yake akiwa na miaka 16, hali iliyomfanya kuwa na mawazo ya kutaka kujitoa uhai.

Bi Holmes anasema aliingiwa na hamu ya kuendesha baisikeli akiwa mtoto mdogo mjini Manchester, wakati baba yake alikua akitumia baisikeli kutoka mji mmoja hadi mwingine kununua viazi kwa gharama nafuu.

''Nakumbuka nilikua nikikalia kiti kidogo karibu na yeye na nyuma yangu kulikua na gunia la viazi'', alisema Holmes.

Baba yake alikua akisoma Iran wakati alipokutana na kumuoa mama yake.

Wakati huo vugu vugu la kupigania mageuzi ya Iran yalikua yameanza na mamlaka ya nchi hiyo ilikomesha malipo ya karo kwa wanafunzi wa nchi hiyo nje ya nchi katika juhudi za kuwataka warejee nyumbani.

''Ni wakati huo baba yangu aliishiwa na pesa na baisikeli iligeuka kuwa kifaa muhimu sana maishani mwake.''

Walihamia Scotland akiwa na miaka miwili ili kutafuta kazi lakini ndoa ya wazazi wake haikudumu na wakaishia kuatengana.

Ishbel na Lucy
Maelezo ya picha, Ishbel akiwa na mbwa Lucy nchini Uturuki

Baada ya hapo maisha yake yalibadilika kwa Bi Holmes.

Nakumbuka nilianza kujihisi vibaya sana, kuona kwamba maisha yangu yamefikia ukingoni, yaani nilijipata najichukia'' .

Bba yake alimtembelea mara moja na baada ya hapo akatoweka kabisa.

''Nilihisi kama ilikua kosa langu baada ya baba kuniacha''Maisha yalikua magumu na mama yake alikua akimlaumu kwa matatizo yote waliopitia.

Uhusiano wake na mama yake ulipozorota alijipata ametengwa na familia na hofu yake ilikua akifikifikisha miaka 16 mama yake hatamhudumia tena.

Siku kadhaa baada ya kutimiza umri wa miaka 16 mama yake alimfukuza nyumbani na kufunga mlango.

''Ni siku ambayo sitawahi kuisahau maishani mwangu'' alisema.

''Nilitembea bila kujua naelekea wapi lakini niliendelea mbele na safari. ''

Hatimae ilijiunga na makao ya watoto lakini aliendelea kuomba Mungu familia yake halisi imruhusi kurudi nyumbani.

Mbwa Lucy kaiwa juu ya baisikeli
Maelezo ya picha, Mbwa Lucy kaiwa juu ya baisikeli

Siku moja akitoka kazini siku ya Jumamosi alikutana na kundi la wanaume ndani ya gari ambao waliomuomba awaoneshe njia.

''Niliingia ndani ya gari lao bila hofu kwa sababu waliahidi kuni rudisha, lakini waliniteka na kunibaka''

''Si kumueleza mtu yeyote masaibu yaliyonikuta na zaidi ya yote nilidhani kwamba ilikua makosa yangu.''

Aliongeza kuwa aliamini alikuwa ana adhibiwa kwa kuwa ''mbaya" na kuendelea kujitenga na watu.

Wakati alipozoea kuwaacha watu wamfanyie vitendo walivyotaka alikua amepoteza kudhulimiwa na kila mtu alikua amejikosesha thamani maishani.

''Nilijichukia kiasi cha kutaka nifilie mbali''.

Alipofikisha umri wa mia 21 alifukuzwa kutoka makao ya watoto na mmoja kati ya wafanyikazi wakuu wa makao hayo alimuuliza kama ataendelea kuishi mitaani.

Swali hilo lilimfanya atafakari upya maisha yake, "siwezi kuendelea kushi hivi".

Alifahamu kuwa ana jukumu la kuamua maisha anayotaka na ni hapo alianza upya kuishi badala ya kuwa na mawazo ya kutaka kujiua.

Ishbel na waendeshaji wengine wa kike wa timu ya Iran
Maelezo ya picha, Ishbel na waendeshaji wengine wa kike wa timu ya Iran

Anakiri kuwa hakuibuka tu siku moja na kuwa mwanamke tajika aliyepata umaarufu wa kuwa mwendesha baisikeli hodari'.

''Ilikua vigumu kuanza upya maish lakini nilijaribu kadri ya uwezo wangu na kurejelea maisha ya kawaida''

Alirejea Uskochi na kujiunga na taasisi ya masomo na hatimae kununua baisikeli iliyomwezesha kuenda chuoni kwasababu ilikua mbali na pia ulikua usafiri wa gharama nafuu.

Pia alijiunga na klabu ya uendeshaji baisikeli mtaani na kuwa mwanamke pekee katika klabu hiyo.

''Napenda kuendesha baisikeli kwasababu inanifanya kusahau mambo mengi, kuwa makini na kujiamini.''anasema Bi Holmes.

Shindano la kwanza kubwa aliloshiriki ni lile la Jumuiya ya madola ambapo alishinda medali ya dhahabu na kuwa Mskochi wa kwanza kuvunja rekodi ya uendeshaji baisikeli katika mashindano hayo.

Ni wakati huo alipata nafasi ya kwenda Iran na alionelea ni vyema kufanya hivyo kwasababu familia yake ilikua huko.

Alipofika mjini Tehran aliombwa kufanya vipimo vya kujiunga na timu ya taifa ya Iran hatua ambayo ilimwezesha kujiunga nao.

"Hii ni nafasi nzuri ya kuunganisha familia yangu."alisema.

Ishbel akiwa Andes Bolivia
Maelezo ya picha, Ishbel akiwa Andes Bolivia

Ni hapo aliamua kuiwakilisha Iran katika mashindano ya jumuia ya Madola nchini Scotland.

Anasema hakuwahi kuzungumzia masuala ya haki ya wanawake lakini alilazimika kufanya hivyo nchini Iran kwasababu hali ya wanawake ilikua mbaya sana.

Nilainza kuzungumzia haki ya waendeshaji baisikeli wanawake na kuangazia jinsi walivyokua wakibaguliwa.

Tulilazimishwa kuvaa hijab katika mazingira ya joto kali. Wachezaji wanawake walipokonywa simu zao tofauti na wachezaji wa kiume.

''Niliambiwa wanafanya hivyo ilikuwazuia kutangamana na wanaume''. Anasema.

Alijaribu kupinga ubaguzi na unyanyasaji huo lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa hadi akaamua kuondoka nchini humo na kuelekea Uturuki amabko alikutana na mwanamume muendeshaji baisikeli ambaye amekuwa akizuru maeneo tofauti kwa kutumia baisikeli yake kwa miezi kadhaa.

''Nilijua wazi kuwa nataka kujiunga nae.

Baada ya kufanya maamuzi alirejea Uskochi na kuuza baadhi ya vitu vyake na kujiunga nae katika mjini Nice, Ufaransa, na kuaza kuzuru maeneo tofauti duniani.

Ishbel hapa ilikua nchini Brazil
Maelezo ya picha, Ishbel amezuru mataifa 20 kwa kutumia baisikeli yake

Kukutana mbwa Lucy

Ilikua nchini Uturuki katika fukwa ya Marmara - alipokutana na Lucy.

Alikua akiendesha baisikeli katika eneo hilo alipomuona mbwa huyo akimkimbiza.

''Nilijiuliza, nitampeleka wapi mbwa huyu wakati mimi ni mwendeshaji baisikeli wa kuzuru mataifa tofauti dniani?''

Alijaribu kuenda mbio lakini mbwa huyo aliendelea kumkimbiza haddi akamfikia.

Alipositisha safari yake ya siku na kutafuta mahali pa kujipumzisha bado mbwa huyo aliendelea kumfuata.

Siku ya pili alijaribu kumrudisha kijijini kwao lakini wakiwa njiani mbwa huyo alivamiwa na ngenge la mbwa koko wengine.

''Nilikumbuka jinsi watu walivyoninyanyasa nikiwa na miaka 16 na sikufanya lolote''

Ni hapo alijipata ameangusha baisikeli yake kando na kupiga mayoe katika juhudi ya kumsaidia umbwa huyo asishambuliwe na bilashaka alifanikiwa kufanya hivyo.

''Nilipiga hatua kadhaa nyuma na kuanza kulia kwa machungu'' lakini anasema hakua anamlilia mbwa huyo bali alikumbuka yale aliyokumbana nayo maishani''

Baada ya hapo mbwa huyo alianza kumfiata tena kurudi walikotoka.

Ishbel with Lucy
Maelezo ya picha, Ishbel na mbwa Lucy

Ishbel aliongeza kuwa alichukua jukumu la kumpatia ulinzi mbwa huyo kwasababu anajua inamaanisha nini kutokua na ulinzi.

Sehemu hiyo ya safari yake ilibadilisha mtazamo wake juu ya maisha - alipata nguvu mpya na ukakamavu wa ajabu baaada ya kupatana na mbwa huyo.

Alijihisi tofauti na kujiambia kuwa hatawahi kunyanyaswa tena, ''nilijiuliza kwanini nilimtetea huyu mbwa lakini sikuweza kujitetea?''

Na kutoka wakati huo aliamua kujipenda na kujithamini japo hakuwa na ufahamu angelifikia vipi hatua hiyo, aliamua kuiga upendo alionao kwa mbwa huyo kujitunza yeye binafsi

Kupitua mbwa huyu naahidi kuwatetea watu wengine wasiokuwa na sauti ya kujitetea duniani''

Taarifa ya Katie Horwich