Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump atishia kufunga mpaka kati ya Marekani na Mexico kutokana na wimbi la wahamiaji
Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kufunga mpaka wa Marekani na Mexico ikiwa Mexico hawatachukua hatua madhubuti kuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.
Hatua hiyo ya kufunga mpaka inatishia kupoteza biashara yenye thamani ya mabilioni ya dola za kimarekani.
Tishio hilo limekuja baada ya kuwepo kwa wimbi kubwa la wahamiaji wanaoingia Marekani wakitokea Mexico kwa nia ya kutafuta hifadhi.
Waziri wa mambo ya nje Marcelo Ebrard amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Mexico ni ''jirani mzuri'' kwa Marekani ''lakini haitachukua hatua kutokana na vitisho''.
Trump alisema nini?
Trump aliwaambia wanahabari siku ya Ijumaa: ''kuna uwezekano mkubwa nitafunga mpaka juma lijalo na hilo kwangu litakuwa sawa tu.''
Alisema ni rahisi sana kwa Mexico ''kuzuia watu kuingia Marekani lakini hawajaamua kufanya hivyo''.
Rais Trump hivi karibuni aliandika mfululizo ujumbe wa twitter ambapo alihitimisha kwa kusema kuwa Marekani ''inapoteza pesa nyingi kwa ajili ya wahamiaji, hasa unaposhughulikia na suala la uingizaji wa dawa za kulevya nakadhalika, kufunga mpaka litakuwa jambo jema!''
Trump pia alitoa maelekezo kukata misaada kwa El Salvador, Honduras na Guatemala ambako wahamiaji wengi hutokea huko.
Lakini hatua hiyo inapaswa kushirikishwa baraza la Congress.
Mexico imesemaje?
Rais López Obrador alisema siku ya Alhamisi kuwa suala la wahamiaji '' si la sisi raia wa Mexico''.
Amesema tatizo hilo limeota mizizi katika eneo la nchi za Amerika ya kati zaidi kuliko Mexico.
''Raia wa Mexico hawatafuti tena kazi nchini Marekani.Wengi wa wahamiaji wana asili ya nchi za Amerika ya Kati''.
Kutokana na kauli ya Trump, Rais Lopez aliambia mkutano kuwa ''Ninataka kuweka wazi kuwa hatutagombana na serikali ya Marekani,''upendo na amani.''
Alizungumzia kuhusu uhamiaji ni ''haki ya mwanadamu'' na kusema kuwa ''watu wa America ya kati hawana namna ya kufanya hivyo hutafuta namna ya kupata maisha bora.
Kwanini Trump anataka kufunga mpaka?
Vyombo vya usalama vilifanya doria na vimekua vikishuhudia idadi kubwa ya watu wanaotafuta hifadhi wakikimbia machafuko El Salvador, Honduras na Guatemala.
Maafisa wa wizara ya mambo ya ndani idadi ya mwezi Machi ilitegemewa kuwa 100,000 idadi kubwa zaidi katika kipindi cha miaka 10 .Zaidi ya wahamiaji 1,000 wakiwa na watoto.
Haijulikani ni kwa namna gani kufunga vituo vya kuingilia kunaweza kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia nchini Marekani, ikizingatiwa kuwa wengi hupitia kwenye vituo visivyo rasmi na kuanza kufuata sheria za kuomba hifadhi wakati tayari wakiwa wameingia kwenye ardhi ya Marekani.
Kufungwa mpaka kunaweza kuathiri uchumi kwenye nyanja za utalii na biashara kati ya Marekani na Mexico, ambayo ilifikia pauni bilioni 469 mwaka jana, kwa mujibu wa ofisi ya sensa ya Marekani.
Ahadi ya kujenga ukuta bado haijatimizwa kwa kuwa baraza la Congress lilikataa kuunga mkono, hata hivyo Trump alitangaza hali ya dharura ili apeleke kwenye ujenzi wa ukuta fedha zilizokusudiwa kupelekwa kwenye jeshi .