Utafiti: Je ni wakati gani ambao mtu anafaa kuitwa mzee?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamke wa umri wa miaka 45 anayeishi Papua New Guinea atahisi kuwa na umri wa miaka 76 nchini Ufaransa ama Singapore.
Na atahisi kuwa na umri kama huo anavyohisi mwanamke wa miaka 65.
Hayo ndio matokeo ya utafiti mkubwa uliofanywa na wanasayansi wa kimataifa na kuchapishwa katika jarida la Lancet.
Watafiti hao walichanganua data ya afya kutoka mataifa 195 na kubaini kwamba kwa jumla watu huwa na wasiwasi wa umri wanapofikisha miaka 65.
Walibaini kuwa matatizo ya kiafya kama vile ukosefu wa kusikia vizuri, mshtuko wa moyo , majeraha ya mara kwa mara na magonjwa ya neva yanaweza kukuathiri katika viwango tofauti vya miaka kulingana na eneo unaloishi.
Na tofauti kati ya wale wanaozeeka vizuri pamoja na wale wanaozeeka mapema inaweza kuwa ya miongo, mitatu ama hata zaidi.

Utafiti huo pia unaangazia mzigo wa magonjwa yanayohusishwa na umri mtu anapozidi kuzeeka .
Utafiti huo unaonyesha kuwa maisha marefu katika umri wa uzee unaweza kuwa fursa ama tishio la idadi ya watu , kulingana na magonjwa yanayohusishwa na afya, kulingana na daktari Angela Y Chang , kiongozi wa utafiti huo.
Watafiti hao walitafuta magonjwa 92, ambayo husababisha madhara katika afya ya maungo na yale ya kiakili . magonjwa mengi ni yale yanayohusisha na moyo na saratani.

Hesabu hiyo imeongezwa kutokana na maeneo ya watu wanayoishi ikizingatia hatua zilizopigwa na kila taifa kimaendeleo
Inatokana na kiwango cha mapato, elimu ,kiwango cha rutba ya uzazi.
Lakini huku mataifa yalioendelea yakiwa na kiwango kifupi cha maisha bado yanahisi athari za kuzeeka .

Je taifa lako linalinganishwaje?
Uchanganuzi huo unaonyesha kwamba magonjwa yanayohusishwa na umri ndio tatizo kubwa la watu wanaozeeka duniani.
Matatizo ya umri yanayosababishwa na umri yanaweza kumfanya mtu kustaafu mapema, kusababisha gharama ya juu ya kimatibabu huku viongozi wa serikali wakitakiwa kuangazia swala hilo wakati watu wanapoanza kuathirika , Chang anaongezea.

Wanasayansi sasa wanatafuta njia za kuzuia sababu zinazoweza kuchelewesha mtu kuzeeka.
Zinaweza kuwa sababu kadhaa kutoka zile za maungo, kuwacha kuvuta sigara hadi mipango bora ya mifumo ya kiafya.
Kuelewa haya ni muhimu katika changamoto za kukabiliana na watu wanaozeeka.













