#FreeOurGirls: Kwa nini watu wanaweka michoro katika picha za rais huyu?

Chanzo cha picha, Twitter/Various
Watumiaji wa mtandao wa Twitter wameunga mkono hatua ya wasichana watatu wa shule kwa kuzichora na kuharibu picha za rais wa Burundi Pierre Nkurunziza wakiiga mfano wao.
Picha zilizoharibiwa za kiongozi huyo zinasambazwa katika mitandao ya kijamii chini ya alama ya reli ya #FreeOurGirls.
Wasichana hao walishtakiwa wiki iliopita wakimtusi kiongozi huyo wa taifa na wanaweza kuhudumia kifungo cha miaka mitano jela.
Mamlaka nchini Burundi hushtumiwa kwa kukabiliana na haki za kibinaadamu na wale wanaopinga serikali.
Wasichana hao walio na kati ya umri wa miaka 15, 16 na 17 walikamatwa wiki mbili zilizopita baada ya picha za rais huyo kuchorwa katika vitabu vya kusoma .
Wanafunzi wengine wanne waliokuwa wamekamatwa pamoja nao waliachiliwa baadaye.
Hizi hapa baadhi ya picha ambazo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni zikiwaunga mkono wasichana hao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1


Chanzo cha picha, @RandomDudeEU

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2

Baba ya mmoja ya wasichana hao aliambia kundi moja la kampeni Human Rights Watch kwamba walikuwa waoga kula.
HRW wameagiza serikali kuwaachilia wasichana hao na kuendelea kukabiliana na matusi yanayofanywa na vikosi hivyo vya usalama.
Mamlaka inafaa kuwakamata wale waliotekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za kibinaadamu badala ya kuwafunga jela wasichana kwa kuchora picha ya rais alisema Lewis Mudge.
Katika kisa kama hicho 2016, wasichana kadhaa walifungwa jela na mamia kufukuzwa shuleni kwa kuzichora picha za rais.













