Rais Donald Trump anadai kuwa ripoti ya mchuguzi maalum Robert Muller ni 'hujuma'

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Marekani Donald Trump amewashambulia vikali mchunguzi maalum Robert Mueller na wakosoaji wake wengine katika kongamano la chama cha Conservative.
Katika hotuba inayotajwa kuwa ndefu zaidi katika utawala wake, bwanaTrump alisisitiza kuwa hana uhusiano wowote na madai ya muingilio wa Urusi katika kampeini yake.
"Tunasubiri ripoti ya watu ambao hawakuchaguliwa'', aliambia umati wa wanachama wa conservative waliyokuwa wakimshangilia.
Bwa Mueller anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa mwendeha mashtaka mkuu muda mfupi ujao.
"Kwa bahati mbaya mnaweka watu wasiyofaa katika nafasi kadhaa za uongozi, na watu wamekuwa wakilalamikia uwepo wao kwa muda mrefu na sasa wanapanga njama ya kukuondoa madarakani sio?" rais alisema.

Chanzo cha picha, Reuters
Mara kadhaa Trump aliashiria kuwa uchunguzi wa mwendesha mashtaka maalum ni "hujuma''
Rais aliwashambulia kina nani?
Akizungumza katika jimbo la Maryland, rais Trump aliwashambulia wakosoaji wake kwa kutumia mameno makali.
"Hivi ndivyo nilivyoteuliwa, kuzungumza bili muongozo maalum . . . na tusipofanya hivyo nchi yetu inaelekea pabaya wenzangu," alianza kusema.
Mara kadhaa rais Trump alisema kuwa Robert Mueller " hakuwahi kuchaguliwa", na kwamba ni naibu mwendesha mashtaka mkuu Rod Rosenstein, aliyemweka Mueller katika nafasi yake.

Chanzo cha picha, Reuters
Kuna madai kwamba, Rosenstein huenda akajiuzulu kutokana na mashambulizi ya rais ya mara kwa mara dhidi yake.
Rais Trump alidai kuwa bwana Mueller alikuwa "rafiki yake mkubwa" huku akimkejeli mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey aliyemfuta kazi mwezi Novemba mwaka jana.
Alisema bwana Sessions alikuwa "alikuwa mdaifu na hakuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wake ilivyostahili".
Rais pia alitaja pendekezo jipya la chama cha Democratic kuhusiana na masuala ya kuimarisha tabia nchi la kulinda kuwa ''wazo la kiajabu''-akisema "upepo utakapoacha kuvuma huo ndio mwisho wa umeme".
Baada ya kugusia masuala kadhaa kuhusu wahamiaji, alisema lazima "tupende nchi yetu",Bwana Trump alisema, "Tuna watu katika Congress ambao hawapendi nchi yetu"
"Najua mnafahamu hilo na tunaweza kuwataja wote kwa majina yao tukiamua kufanya hivyo," alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia alitetea mkutano wake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un, na kusema kuwa "wamepiga hatua kubwa ".
Hotuba hiyo inakuja wiki moja baada ya wakili wake wa zamani Michael Cohen, kudai kwamba kiongozi huyo alimtaka adanganye kuhusu kuhusu biashara ya ujenzi wa jengo mjini Moscow wakati wa kampeni ya uchaguzi wake.














