FBI ilishangazwa na hatua ya Trump kumfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey

Rais wa Marekani Donald Trump

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Donald Trump
Muda wa kusoma: Dakika 2

Ikulu ya White House imelaani vikali ripoti ya gazeti la New York Times kwamba shirika la ujasusi la Marekani FBI lilianzisha uchunguzi kubaini ikiwa Trump alikuwa akiifanyia Urusi kazi kisiri.

Maafisa hao wa utekelezaji wa sheria walishangazwa na mwenendo wa bwana Trump mwezi Mei 2017, alipomfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey.

Uchunguzi huo ulihusisha kutathmini kama Trump ni tishio kwa usalama wa taifa.

"Hili ni jambo la kushangaza,"alisema Sarah Huckabee Sanders msemaji wa Ikulu ya Marekani.

"James Comey alifutwa kazi kwasababu alivunja kanuni ya kazi yake," ilisema taarifa yake.

"Tofauti na rais Obama, aliyeacha Urusi na mahasimu wengine kuidhalilisha Maerekani, Rais Trump amechukua hatua."

Mwaka 2016, Mashirika ya ujasusi ya Marekani yalithibitisha kuwa Urusi iliingilia kati uchaguzi wa uraisi wa taifa hilo.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

FBI ilichunguza nini?

Gazeti la New York Times linadai kuwa uchunguzi huo ulijumuishwa katika uchunguzi wa FBI uliyokuwa ukiongozwa na bwana Robert Muller kuhusu uwezekano wa Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2016 na uhusiano wowote wa Trump kwa suala hilo.

Rais Trump mara kwa mara amekana kuwa ushirikiano wowote na Urusi.

Mkurugenzi wa zamani wa FBI James Comey alitoa ushahidi kwamba Trump alimtaka kuwa mtiifu na mwaminifu huku akimuomba kufutilia mbali uchunguzi wa aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama Michael Flynn.

Mnamo mwezi Desemba mwaka 2017 Flynn, alikiri kwamba aliandikisha taarifa ya uongo kwa idara ya uchunguzi wa jinai ya Marekani, FBI.

Rais Trump mara kwa mara amekana kuwa ushirikiano wowote na Urusi.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais Trump mara kwa mara amekana kuwa ushirikiano wowote na Urusi.

Hatua hiyo ilimfanya ashurutishwe kujiuzulu mwezi mmoja baadae kwa kupotosha Ikulu ya White House kuhusu mkutano wake na balozi wa Urusi kabla ya Trump kuingia madarakani.

Mashtaka dhidi yake yaliwasilishwa na mwanasheria maalum Robert Mueller kama sehemu ya uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016.

Gazeti hilo linasema kuwa uchunguzi huo uliendelezwa FBI chini ya Robert Mueller ambaye aliajiriwa siku chache baada yaComey kufutwa

Trump amekanusha madai ya yeye kushirikiana na Urusi na kutaja uchunguzi wa Mueller "kama hujuma ya kisiasa".

Kando na hayo, uchunguzi huo uliwahusisha wandani wa karibu wa rais Trump na hata baadhi yao kujipata kizimbani.

Mwanasheria zamani wa rais Donald Trump, Michael Cohen alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kupatikana hatia ya matumizi mabaya ya fedha za umma na uvunjifu wa sheria za uchaguzi.

Gazeti la Times halikubaini ikiwa FBI bado inaendesha unaendesha uchunguzi dhidi yake kuhusiana na suala la muingilio wa Urusi katika Uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 2016

Gazeti hilo linasema kuwa liliona majina ya wanasheria wazamani aambao hawakutajwa jinaT, "wengine wanafahamu uchunguzi huo," na ushahidi wa pamoja wa kundi la washauri wa zamani wa FBI James. M Baker..