Hakuna silaha kwa polisi wasio kazini Burundi

Amri imetolewa na maafisa nchini Burundi kwa polisi kutokuwa na silaha au kuvalia sare za polisi ambao hawako kazini.

Makao makuu ya polisi nchini Burundi yamepiga marufuku ubebaji wa silaha na uvaaji wa sare za polisi kwa polisi wakati wanapokwenda kwenye vilabu vya pombe au mahali pengine popote kunakouzwa vileo .

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya watu wanne kuuawa kwa bunduki katika kitongoji cha Gatumba yapata kilomita 15 magharibi mwa mji mkuu Bujumbura na polisi waliokuwa wamelewa mwishoni mwa juma.

"Hakuna afisa wa polisi anayeruhusiwa kubeba guruneti vinginevyo atahesabiwa kama muhalifu na afisa yeyote wa polisi atakayekwenda kwenye baa na silaha lazima ataadhibiwa kikamilifu ,"ulisema waraka wa Mkuu wa polisi aliousaini Ijumaa.

Miongoni mwa watu waliouawa, alikuwa ni afisa wa polisi wa eneo hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Makao makuu ya polisi, ni marufuku pia kwa polisi kubeba gurunadi na kilipuzi cha aina yoyote ile.

Polisi pia hawaruhusiwi kwenda likizo na silaha.

Kwanini hatua kuidhinishwa?

Tangu kuibuka kwa mzozo mwaka 2015, polisi waliweza kwenda vilabuni hata wakati wako likizo na silaha zao kwa sababu za usalama.

Lakini sasa, matukio wakati ambapo polisi wanawauwa raia yanaonekana kuongezeka.

Mwezi uliopita, polisi alimfyatulia risasi mwendesha baiskeli mjini Bujumbura, ambaye alikufa uwanjani.

Afisa wa polisi alichukua bunduki aina ya Kalashnikov baada ya fujo za mapigano ya jumla na kufyatua risasi kiholela, kulingana na mtu aliyeshuhudia tukio hilo ambaye alinusurika na kuzungumza na shirika la habari la AFP.

Mauaji yalitokea siku moja baada ya agizo lililotolewa kutoka kwa Ispekta Mkuu wa Polisi, Merchiade Rucekequi, aliwazuwia maafisa wa polisi kutembea na gurunadi kwenda kwenye var "in duty clothes and weapons".

Nchini Burundi,polisi wanajihami kwa silaha. Hubeba silaha aina ya machine guns, guruneti , na mara nyingi hupatikana katika visa vya mauaji na wizi wa kutumia silaha.