Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Moto Mt. Kenya: Wakulima wa bangi watuhumiwa kuwasha moto
Moto unaodaiwa kuwashwa na wakulima wanaotaka kupanda bangi unatishia maelfu ya mahekari ya misitu ya mianzikatika Mlima Kenya au Mount Kenya.
Tayari moto huo umeharibu kilomita 80 mraba za ardhi yenye nyasi na sasa unatishia misitu ya jadi.
Misitu mikubwa ya mianzi inapatikana katika eneo la Afrika mashariki.
Kwa mujibu wa shirika la utafiti wa kimataifa wa ukulima CGIAR, ni sawa na takriban 3-4% ya misitu jumla ya mianzi au bamboo inayojulikana.
Moto huo, ulianza siku saba zilizopita, unateketea katika maeneo mawili na umekuwa ukisambaa kutokana na upepo na joto kali.
Shirika la Wanyama pori limeeleza kwamba limekuwa likiendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo, na kwamba maafisa wa zima moto wamepiga kambi katika eneo hilo wakiendelea na jitihada za kuuzima moto.
Wanasaidiana na maafisa kutoka kikosi cha ulinzi KDF.
Watu wa jamii kutoka eneo hilo wamekuwa wakisaidiana na maafisa wa misitu na mashirika ya kibinafasi ya kuhifadhi mazingira, ambao wana rasilmali msingi kukabiliana na ukubwa wa moto huo.
Wakulima wanatuhumiwa kuuwasha moto huo wanoajaribu kulisafisha eneo la ardhi ili kupanda bangi na sasa unatishia mojawapo ya maeneo matano ya juu linalofahamika kama "water towers", ambalo ni chanzo cha maji kwa mito na ndio chanzo cha robo tatu ya maji yanayosambazwa nchini.
Moto katika eneo jingine unatishia misitu ya mianzi yenye ukubwa wa hekari 40,000.
Mount Kenya ni mlima wa pili kwa urefu barani Afrika.
Picha za Bobby Neptune