Rais Buhari anaongoza kwa kura za majimbo dhidi ya mpinzani wake mkuu Atiku Aboubakar

Chanzo cha picha, Reuters/AFP
Rais Muhammadu Buhari anaongoza katika matokeo ya awali yanayoendelea kufuatia uchaguzi Mkuu nchini Nigeria ,Anaongoza majimbo manne kati ya 36.
Buhari amechukua majimbo mawili kusini Magharibi,moja Mahariki na katikati mwa Nigeria,Huku Mpinzania wake Atiku Abubakar akiongoza mji mkuu wa nchi hiyo Abuja.
Wakati matokeo ya awali yakiendelea kutangazwa wafuasi wa Abubakar kutoka chama cha People's Democratic Party (PDP) wamedai kumekua na makosa katika kura hizo
Mwenyekiti wa chama cha upinzani ameuita uhesabuji huo wa kura kua "Sio Sahihi na Haukubaliki".
Amedai kua kumekua na njama za serikali ya Raisi Buhari na washirika wake kutaka kufanya udanganyifu", Lakini hakuweza kutoa ushahidi kuhusu ulaghai huo
"PDP inalazimishwa kutanganza na kuwa na upande kwasababu sasa demokrasia yetu ipo hatarini, mbali na njama za kutaka kuharibu mchakato wa uchaguzi, nataka niwatoe wasiwasi wafuasi wetu kuwa PDP iko njiam kushinda katika uchaguzi huu, tunataka uongozi wa tume ya uchaguzi, hasa hasa mwenyekiti, watende haki na sio kuharibu demokrasia, kwasababu dunia inatazama.

Chanzo cha picha, Getty Images
Umoja wa Ulaya ,Marekani na Umoja wa Afrika wameonesha hisia zao kuhusiana na kuendelea kucheleweshwa kwa matokeo pamoja na uwepo wa Dosari katika uchaguzi wa siku ya Jumamosi,Lakini hakuna waangalizi waliosema kua kumekua na wizi wa kura
Buhari, Mwanachama wa chama cha All Progressives Congress (APC) party, anatetea kiti chake katika muhula wa pili huku akikabiliana na upinzani mkalu kutoka kwa Bwana Atiku Abubakar.
Vyama vyote vimekua vikilalamika kua chama kingine kimekua na ushirika wa karibu na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo (Inec) kushinikiza Uchaguzi, Ambao hapo awali ulifaa kufanyika tarehe 6 February lakini uliahirishwa masaa machache kabla ya siku husika .Hakua chamba kinachoendeleza madai hayo kwa sasa.
Buhari Ameiahidi kuipeleka Nigeria kwenye hatua nyingine na kusema kua ataendeleza yale aliyoyafanya awamu yake ya kwanza,Huku mpinzani wake Mfanyabiashara mkubwa nchini Nigeria Bwana Abubakar, amekua akimshutumu rais Buhari kwa kuupoteza muhula wake ofisini na kuahidi kua atalifanya taifa hilo kurudi katika mstari.
Mbali na Buhari kuchukua majimbo manne na Abubakar Akishinda katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja ,Inaonesha pia Buhari ameshinda jimbo ya Yobe ukanda wa kaskazini Mashariki ,Huku Atiku Abubakar akichukua kusini Magharibi mwa jimbo la Ondo.

Chanzo cha picha, AFP
Matokea rasmi huenda yasitangazwe mapema kama yalivyotazamiwa mpaka kufikia juma lijalo. Lakini Mwenyekiti wa chama cha PDP Bwana Secondus Tayari amekosoa uhesabuji kura wa awali akishutumu chama tawala kua wamekua wakitumia mashtaka,kudanganya,Kufungwa jela ili kushinikiza matokeo.
Ameiambia ripoti kua itakua ni vigumu kwa Nigeria "kukubali hatua hii ya vitisho".
Hata hivyo shirikisho la kiserikali limekishutumu chama cha PDP kwa kujaribu kupinga na kusababisha migogoro ya kikatibaisis. Lai Mohammed,Waziri wa Habari na utamaduni amesema kua PDP wameonesha uvunjifu wa hatua za upigaji kura.
Wagombea hawa wawili wametoka kwenye eneo la watu wa dini ya kiislamu ukanda wa Kaskazini mwa Nigeria. Wote ni wenye miaka zaidi ya 70,huku nusu ya watu milioni 84 waliojiandikisha kupiga kura ni chini ya miaka 35.













