Wamuokoa mbwa mwitu kutoka kwenye barafu wakidhani na mbwa

A grey wolf stares straight into the camera with a muzzle on its snout, lying on the floor of a vet's office

Chanzo cha picha, EUPA

Maelezo ya picha, 'Mbwa' huyo alipelekwa kwenda

Wasamaria wema nchini Estonia wamefika kumuokoa waliyedhani ni mbwa aliyetaabika baada ya kukwama katika mto ulioganda barafu - pasi kufahamu kuwa wanamuokoa mbwa mwitu na kumuingiza ndani ya gari.

Wanaume hao walikuwa wakifanya kazi katika bwawa la Sindi katika mto wa Parnu walipomuona mnyama huyo aliyekwama kwenye maji ya barafu.

Baada ya kusafisha njia kwenye theluji, walimpeleka mnyama huyo hadi kwenye kituo cha afya cha kuwahudumia wanyama kupata usaidizi.

Ni hapo ndipo walipoarifiwa kwamba wamembeba mbwa mwitu.

This photo shows the wolf with ice frozen all over its fur in an outdoor setting, having just been pulled from the river - a human's hands can be seen wrapping it in a towel

Chanzo cha picha, EUPA

Maelezo ya picha, Alikuwa amefunikwa kwa theluji kutoka mto huo ulioganda barafu

Muungano wa Estonia wa ulinzi wa wanyama (EUPA) amesema mbwa mwitu huyo alikuwa na shinikizo dogo la damu alipofikishwa katika hospitali hiyo ya wanyama, ambayo huenda ikaelezea kudhoofika kwake, na kwanini kinyume na kawaida, hakuwashambulia waokozi wake, baada ya jamaa hao kumbeba na kumuingiza kwenye gari ili apate joto.

"Ilibidi tumbebe kutoka mlimani, alikuwa na uzito sio haba."amesema Rando Kartsepp, mojawapo ya jamaa waliomuokoa mnyama huyo.

"Alikuwa ametulia, alilala miguuni mwangu. Nilipotaka kuyanyoosha, aliinusha kichwa chake kidogo," aliongeza.

Madakatari walikuwa na shaka, kuhusu uhalisi wa mbwa huyo, lakini muindaji wa eneo hilo, ambaye anawafahamu mbwa mwitu kutoka eneo hilo , ambaye hatimaye alithibitisha kwamba kweli alikuwa mbwa mwitu, aliye na umri wa mwaka mmoja hivi.

"Alikuwa ametulia, alilala miguuni mwangu'' amesema Kartsepp

Chanzo cha picha, EUPA

Maelezo ya picha, "Alikuwa ametulia, alilala miguuni mwangu'' amesema Kartsepp

Badaa ya kupata taarifa hii, maafisa katika kituo hicho cha afya waliamua kumuweka kwenye kizuizi baada ya kumtibu - iwapo angepata nguvu na achangamke baada ya kupona.

Aliponea mkasa huo uliomfanya nusra kupoteza maisha yake baada ya siku moja na baada ya kubandikwa kifaa cha kujua anakwenda sehemu gani, aliachiliwa huru kwenda msituni.