Kepa Arrizabalaga: 'Hujuma kwa Chelsea' baada ya kipa kukataa agizo la Maurizio Sarri katika fainali ya Carabao

Maurizio Sarri and Willy Caballero

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maurizio Sarri alikuwa anataka kumuingiza Willy Caballero

Je umewahi kuhsuhudia kitukama hichi?

Mchezaji akataa kuondoka uwanjani - na meneja wake apoteza muelekeo wa mechi.

Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga alikataa jitihada za meneja Maurizio Sarri kumbadilisha uwanjani katika dakika za ziada za mechi ya fainali ya kombe la Carabao, hatua iliomuacha meneja huyo akiwa na hasira kubwa nje ya uwanja huo.

Arrizabalaga alikuwa amehudumiwa kwa kubanwa kwa maumivu ya msuli, na wakati mechi ikiwa 0-0, Sarri alikuwa anajitayarisha kumuingiza kipa wa akiba Willy Caballero katika nafasi ya Kepa kabla ya awamu ya mikwaju ya penalti.

Lakini baada ya kunyosheana vidole kwa muda kadhaa na kupiga kelele, HAPANA!, ilibidi Sarri asalimu amri.

Refa Jonathan Moss alikimbia kumfuata Sarri kuthibitisha iwapo kweli anataka Arrizabalaga aondoke au la, na Sarri, ilibidi abadili msimamo wake kabla ya kuondoka kwa hasira , na muda mfupi baadaye kurudi, akimuacha kipa wa akiba Caballero akiwa amechanganyikiwa.

David Luiz and Kepa Arrizabalaga

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mlinzi wa Chelsea David Luiz ajaribu kumtuliza Kepa Arrizabalaga uwanjani

Arrizabalaga alifanikiwa kuokoa mkwaju wa Leroy Sane - lakini Raheem Sterling alifunga bao la ushindi katika mikwaju hiyo ya penalti wakati Manchester City walipotuzwa mabingwa wa taji hilo la Carabaokwamwaka wa pili kutokana na ushindi wa mwisho wa mabao 4-3.

Sarri hakuonekana kuonyesha hisia zozote, wakati wachezaji wake wakionekena kuhuzunishwa kwa kushindwa.

'Ni hujuma kwa Chelsea' - uchambuzi

Aliyekuwa mshambuliaji huko Stamford Bridge Chris Sutton ameeleza matukio ya jana kama ''hujuma kwa Chelsea" na kuapa kwamba Arrizabalaga "hastahili kucheza tena katika klabu hiyo".

Hilo linajiri kufuatia wiki kadhaa za uvumi kuhusu nafasi ya Sarri kama meneja wa klabu hiyo na wasiwasi kuhusu mbinu zakezilizopewa jina maarufu "sarri-ball".

"Kama ningekuwa Sarri ningeondoka. Huwezi kudharauliwa. Ni kwanini wachezaji hawakumburura Kepa nje?

"Kepa anastahili kufutwa kazi, sio Sarri. Amedhauriliwa - sio jambo zuri kwa meneja."

Aliyekuwa mchezaji wa England na timu ya Tottenham Jermaine Jenas anasema ni wazi "hakuna heshima" kwa meneja, lakini amesema Sarri ameonyesha "hana ustaarabu" kwa kuamua kuondoka uwanjani baada ya kushindwa.

Mambo yalivyoitukia...

Chelsea keeper Kepa Arrizabalaga struggles with cramp

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga abanwa na maumivu ya msuli karibu mwisho wa muda wa ziada
Willy Caballero is ready to come on for Chelsea

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kipa wa akiba Willy Caballero yuko tayari kuingia uwanjani
Arrizabalaga saying he doesn't want to go off

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Arrizabalaga ampigia kelele meneja wake, hataki kuondoshwa uwanjani
Maurizio Sarri shouting at Kepa

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Maurizio Sarri amjibu kwa hasira Arrizabalaga huku msaidizi wake Gianfranco Zola akishangazwa
Maurizio Sarri and Jonathan Moss

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Refa Jonathan Moss amuuliza Sarri iwapo anataka kumtoa kipa wake
Maurizio Sarri storms down the tunnel

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Sarri anaondoka uwanjani na kipenga kinapulizwa kumalizika muda wa ziada