Uchaguzi Nigeria 2019: Mambo matano kuhusu Nigeria

Chanzo cha picha, AFP
Zaidi ya raia milioni 84 wa Nigeria wanajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu Februari 16, lakini unafahamu nini kuhusula Afrika lenye idadi kubwa zaidi ya watu na uchumi mkubwa?
1) Mtindo wa kiafrika - Unachangia fedha za kigeni
Wanamuziki wa Nigeria wanazuru kila pembe ya dunia kuwatumbuiza mashabiki wao kwa miondoko ya kuvutia ya kiafrika ambayo imewazolea tuzo mabalimbali.
Hii haifai kufananishwa na mtindo wa kiafirika iliyokuwa ikichezwa na mwanamuziki nguli wa miondoko hiyo Fela Kuti - ambaye aliiweka kileleni Nigeria miaka ya 1970 na 1980, kwa kuchanganya mitindo tofauti ya kitamaduni, funk na jazz.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wasani wengine wa kimataifa kama vile Wizkid, Davido, Tiwa Savage na Jidenna, wamedhihirisha kuwa muziki ni kiungo muhimu inayoiletea Nigeria fedha za kigeni - kiasi cha kuzifanya kampuni kubwa za muziki duniani kama vile Universal Music Group na Sony kufungua ofisi zao nchini humo.
Wimbo wa Davido kwa jina Fall, kilichotolewa mwaka 2017, ndio muziki wa Nigeria uliyo na video maarufu zaidi- ulitazamwa zaidi ya mara milioni moja katika mtandao wa Yotube na bado unafuatiliwa.
"Miondoko ya wasanii kutoka Afrika magharibi imetawala bara zima la Afrika, na inachezwa sana katika vilabu vya burudani na maredioni," DJ Rita Ray aliiambia BBC.
"Mtindo wa Afrobeat pia imewavutia wasanii wa muziki ya RnB kama vile Ed Sheeran na wale wa Rap Drake na Stefflon Don,ambao wameijumuisha katika kazi yao ya hivi karibuni.
Pia tusimsahau msanii na mtunzi wa muziki MNEK mwenye asili ya Uingereza na Nigeria, ambaye anajivunia kufanya kazi na wasanii tajika duniani.
Mitindo hiyo imejumuisha miondoko ya pop ya kiafrika ya Nigeria na Ghana ambayo ilifahamika kama hiplife, azonto na dancehall - ni kibao cha Oliver Twist chake msanii D'banj ambacho kilizindua rasmi mtindo wa Afrobeat mwaka 2012, na kilipanda hadi nambari tisa katika chati ya muziki nchi Uingereza, alisema.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe
Wasani wengine wa Nigeria ambao pia wameimarisha muziki wa Afrika kutoka nchini humo ni Yemi Alade, Tekno, Falz, Olamide, Simi, Mr Eazi, Mologo na Patoranking.
"Kile kinachofanya Afrobeat kuvutia ni mtindo wake wa densi- Wanigerian wanafahamika kwa mitindo hiyo ya densi ambayo imechangia pakubwa kuimarika kwa muziki wao," anasema Rita Ray.
2) Waandishi maarufu
Kando na muziki Nigeria pia inajivunia waandishi maarufu wa vitabu kama vile marehemu Chinua Achebe, ambaye kitabu chake Things Fall Apart kimeuza zaidi ya nakala milioni 20 tangu kilipochapishwa mwaka 1958.
Kitabu hicho pia kimetafsiriwa katika lugha 57. Wole Soyinka alikuwa mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Nobel ya uandishi mwaka 1986 huku kitabu The Famished Road cha Ben Okri kikishinda tuzo mashuhuri ya Man Booker mwaka 1991.

Chanzo cha picha, AFP
Waandishi kama vile Chigozie Obioma, Helon Habila, Chibundu Onuzo Sefi Atta na Adaobi Tricia Nwaubani miongoni mwa wengine bado wanaendeleza utamaduni wa watangulizi wa kushinda mattuzo tofauti kutokana na kazi zao za kusifika.
"Wanageria wanapenda kuonekana na kusikika. Huenda kuna mamia ya wengine ambao wananasimulia hadithi za kusisimua kutoka barani, lakini wanaigeria wanaangaziwa zaidi kutokana na ukakamavu wao," Nwaubani aliiambia BBC.
"Lengo letu ni kuongoza katika kila kitu tunachofanya. Tunahakikisha kila mmoja anajua tumeingia ukumbini. Hata baadhi ya wenzetu ambao kazi zao hazijatambulika nje ya nchi wanahakikisha kazi yao inatambulika."
Utamaduni wao wakusherehekea kila hatua ya maisha tangu jadi umechangia uvunifu wao wa kusimulia hadithi tofauti.
Wakati sekta ya filamu yenye thamani ya mamilioni ya madola milioni, inayofahamika kama Nollywood, ni ishara wazi kuwa wana ubunifu mkubwa
Mtetezi wa masuala na nafasi ya wanawake katika jamii katika karne ya 21 ni mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie, ambaye ameangazia masuala hayo kwa ustadi mkubwakatika kitabu chake Dear Ijeawele: "The knowledge of cooking does not come pre-installed in a vagina."
3) Wanakuza mafuta kwa wengi, lakini umeme ni haba
Licha ya kuwa Nigeria inakuza mafuta kwa wingi barani Afrika ambayo inaipatia fedha za kigeni, wanaigeria wengi wanaamini utajiri wao wa mafuta umefujwa kwa mika mingi.

Chanzo cha picha, AFP
Uzalishaji wa umeme umeongezeka tangu mwaka 2000 lakini serikali imekuwa ikikabiliwa changamoto ya kukidhi mahitaji kutokana na ogezeko la idadi ya watu kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kawi.
Uzalishaji wa umeme haujabadilika pakubwa nchini Nigeria tangu mwaka 2005 kwasababu kuanzia wakati huo idadi ya watu imeongezeka kwa karibu milioni 57, ambayo ni sawa na idadi ya sasa ya watu nchini Afrika kusini.
Ni nusi ya watu wote wa Nigeria ambao wana umeme majumbani mwao,na hali ni tofauti kati ya wakaazi wa mijini na vijijini.
4) Nyumbani kwa Boko Haram
Hashtag ya #BringBackOurGirls ilipata umaarufu mkubwa duniani kufuatia kisa cha utekaji nyara wa wasichana wa shule ya Chibok na wanamgamo wa Boko haram.
Utekaji huo ulifanyika mwaka 2014 ambapo zaidi ya wasichana 200 wa shule ya Chibok, Kaskazini mashariki ya Nigeria na mpaka sasa hwajapatikana.

Chanzo cha picha, AFP
Kundi hilo lilibuniwa mwaka 2002 katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri, ambapo wakaazi waliipatia jina la Boko Haram, ambayo inamaanisha eneo la jamii ya watu wahausa ambako"Elimu ya magharibi imepigwa marufuku".
Kihistoria, viongozi wa kidini kaskazini mwa Nigeria walipinga utawala wa wakoloni wa Uingereza. Lakini Andrew Walker,mwandishi wa kitabu kuhusu Boko Haram, kinachofahamika kama"Eat the Heart of the Infidel", anasema kuna sababu kubwa zaidi ya hilo.
"Kumekuwa na historia ndefu ya itikadi kali ya kidini kaskazini mwa Nigeria," aliiimbia BBC. "Hivi karibuni suala la wanasiasa wafisadi sio waislamu lilitumiwa na kiongozi wa kidini sheikh Mohammed Yusuf kuzindua Boko Haram.

Chanzo cha picha, AFP
Kifo cha bw. Mr Yusuf mikononi mwa polisi karibu muongo mmoja uliyopita uliifanya kundi hilo kuanzisha oparesheni ya kijeshi ya kubuni jimbo kiislamu.
Maelfu ya watu walitekwa na kuingizwa katika kundi hilo huku jimbo lililokaliwa na wanamgambo hao likiongozwa kupitia sheria ya kislamu.
Mwaka 2015, kundi la Boko Haram liliorodheshwa kuwa kundi hatari zaidi la kigaidi duniani na Taasisi ya masuala ya uchumi na amani duniani.
5) Inakaribia kuishinda Marekani kwa idadi ya watu
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa kufikia mwaka 2047 Nigeria itakuwa imepita Marakani kwa idadi kubwa ya watu.

40% ya watu 196 million nchini Nigeria wako chini ya miaka 14 ikizingatiwa kuwa vijana wanamchango mkubwa katika uchaguzi huu inaarifiwa kuwa zaidi ya nusu ya wale waliyojiandikisha kupiga kura wako chini ya miaka 35.















