Mahakama Bangladesh yawashikilia wanaume saba kwa ubakaji

Chanzo cha picha, NURPHOTO/GETTY
Mahakama nchini Bangladesh imewaweka kizuizini wanaume saba akiweko kiongozi mmoja wa ngazi ya chini wa chama kinachotawala nchini humo cha Awami League, kuhusiana na tuhuma za ubakaji.
Mama wa watoto wanne anadaiwa kubakwa na kundi la wanaume kutokana na kwamba alipigia kura chama cha Upinzani cha Bangladesh Nationalist Party, katika uchaguzi ulioganyika wiki iliyopita.
Shambulio hilo lililofanyika wakati wa uchaguzu, limesababisha maandamano na hasira katika mitandao ya kijamii.
Hata hivyo wanaume hao wamekanusha madai hayo, na kiongozi huyo wa ngazi ya chini aliyehusika na ubakaji. Amefukuzwa katika chama.

Chanzo cha picha, EPA
Chama cha Awami kimepata ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika Jmapili iliyopita, ambao ulijawa na vurugu, vitisho na madai ya kuwepo kwa hila katika uchaguzi huo, uliouwa watu 17 wafuasi wa chama tawala na upinzani.
Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake juu ya kile ilichokielezea kama ulipizaji visasi dhidi ya upinzani wa kisiasa unaofanywa na wanaharakati wa chama tawala baada ya uchaguzi.
Mume wa mwanamke huyo alitoa malalamiko wiki iliyopita akisema kuwa kundi la wanaume liliwavamia nyumbani kwake katika wilaya ya Noakhali na kumfunga yeye na watoto wao wanne na kisha wakambaka mkewe, usiku wa manane.
Baada ya wabakaji hao kuondoka jirani walitoa msaada na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 35, kupelekwa hospital.
Taarifa za awali zinasema mwanamke huyo alionywa mapema alipokuwa katika kituo cha kupiga kura kwamba asimpigie mgombea wa upinzani.













