Kanisa kubwa zaidi Mashariki ya Kati lafunguliwa Cairo, Misri - Trump afurahia

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ameongoza ufunguzi wa kanisa jipya la Coptic lililojengwa mashariki ya mji mkuu Misri, Cairo.
Kanisa hilo kuu jipya liliendesha misa yake ya kwanza chini ya ulinzi mkali jumapili ya mkesha wa krismasi ya Coptic.
Siku ya Jumamosi, afisa mmoja wa polisi aliuawa alipokuwa akijaribu kuondoa kilipuzi kilichokuwa kimefichwa kwenye paa la nyumba katika mji wa Nasr viungani mwa mji mkuu wa Cairo.
Waumini wa madhehebu ya Coptic ni 10% ya raia wote nchini Misri ambako idadi kubwa ya watu ni Wislamu.
Wenge wanasema serikali inawabagua na kwamba haiwapatii ulinzi wa kutosha.

Chanzo cha picha, EPA
Bwana Sisi, ambaye alijitangaza kuwa mlinzi wa wakristo dhidi ya makundi ya watu wenye misimamo mikali, aliliwaambia waumini kuwa ufunguzi wa pamoja wa Kanisa hilo kuu jipya na msikiti wa Al-Fattah Al-Aleem ni ishara ya umoja wao.
"Sisi ni wamoja na tutasalia kuwa pamoja,"Bwana Sisi alisema akifungua kanisa hilo akiashiria waumini wa dini ya Kikristo na Kislam nchini Misri.
Rais wa Marekani Donald Trump ameandika kwenye Twitter: "Nafurahia sana kuwaona marafiki zetu wa Misri wakifungua kanisa kubwa zaidi Mashariki ya Kati. Rais El-Sisi anaongoza taifa hilo kwenye siku za usoni za kuwajumuisha wote!"
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Chanzo cha picha, EPA

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Papa Francis alitoa salamu za heri njema kwa Papa Tawadros II Alexandria,ambaye ndiye mkuu wa kanisa la Coptic, baadaye aliongoza misa.

Chanzo cha picha, EPA

Chanzo cha picha, Reuters
Msikiti mpya wa Al-Fattah Al-Aleem ni mkubwa mara mbili ya kanisakuu jimpya na mijengo yote ya ibada iko katika mji mkuu wa Misri Cairo

Chanzo cha picha, EPA

Chanzo cha picha, EPA
Picha zote ziko na haki miliki













