Januhairy: Kwa nini wanawake wanakuza nywele zao mwezi huu

Chanzo cha picha, LAURA JACKSON
Kwa mara ya kwanza kampeni ya kuwasisitiza wanawake kukuza nywele zao mwilini imefanyika.
Kampeni hii inayojulikana kama 'Januhairy' inawataka wanawake kuzipenda na kuzikubali nywele zao halisi huku wakiwa wanachangisha fedha kwa ajili ya wahitaji.
Mhasisi wa kampeni hii Laura Jackson, mwenye umri wa miaka 21 amesema kuwa amepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanawake duniani kote ambao wako tayari kushiriki katika kampeni hiyo.
Mwanafunzi wa chuo cha Exeter alisema kuwa alikuja na wazo hilo baada ya kukuza nywele zake kwa ajili ya maonyesho.

Chanzo cha picha, LAURA JACKSON
"Licha ya kuhamasika na kujiamini mwenyewe, baadhi ya watu wanaonizunguka huwa hawanielewi au kukubaliana na mimi, kwa nini huwa sinyoi", mwanafunzi mmoja wa mwaka wa tatu alisema.
" Nimegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo yanahitajika kufanyika ili tuweze kukubaliana kiukweli kati ya mtu na mtu", mwanafunzi huyo aliongeza.
Kampeni hiyo ilizinduliwa mwezi uliopita na sasa wanawake kutoka Uingereza,Marekani,Canada, Ujerumani,Urusi na Uhispania wanashiriki.
Bi.Jackson kutoka Kineton, ana matumaini ya kuchangisha Euro 1,000 kwa ajili ya wahitaji kutokana na mpango huo uliovuma kuhusu elimu ya mwili, ambao unawafundisha vijana kuhusu picha ya mwili.
"Ninataka wanawake wajisikie huru wakiwa katika uzuri wao wa kipekee wa miili yao",

"Hii sio kampeni ya hasira kwa watu ambao hawaoni umuhimu wa nywele za kawaida za mwili ulivyo.
Ni kampeni ambayo inawezesha miradi ya kila mtu kuelewa zaidi kuhusu maoni yao juu yao wenyewe na watu wengine, Bi. Jackson alisema.."
" Nadhani kuwa nywele zisiwafanye wanawake kujiona kuwa hawajakamilika ," alisema India Howland mwenye umri wa miaka 22, kutoka Lymington.
"Nimewahi kuwasikia wasichana wakiomba radhi kwa kuwa na nyewle miguuni, lakini hakuna mtu ambaye anamlazimisha kuzinyoa . Ni matakwa ya mtu", mwanafunzi mwingine wa mwaka watatu alisema.













