'Mwanangu amelelewa katika mazingira ya kuishi na chui tangu alipokuwa mtoto mdogo'

Tiago na wanyama

Chanzo cha picha, Family handout

Maelezo ya picha, Picha hii ya Tiago akiwa karibu na wanyama hatari imezua gumzo mitandaoni, huku baadhi yao wakitiliashaka uhalisia wake

Picha inayomuonesha mvulana mdogo akiwa karibu na chui wawili ndani ya maji inaendelea kuzua gumzo katika mitandaoni ya kijamii

Umaarufu wa picha hiyo umezua maswali kuhusiana na uhalisia wake.

Hata hivyo, picha hiyo ni ya kweli kama inavyobainisha na BBC.

Tiago Silveira, kijana anayeonekana katika picha hiyo ameishi na kucheza na chui hao tangu alipokuwa mtoto mdogo nchini Brazil.

"Baadhi ya marafiki zangu huniambia picha hiyo si ya ukweli, lakini watu wengi wanaipenda na wao pia wanataka kukutana na chui hao. Ni vyema kuwaonesha watu maisha yangu ya kuishi na wanyama kwasabahu wao hawajabahatika kama mimi,"kijana huyo wa mika 12 aliiambia BBC News Brasil (Idhaa ya Kireno ya BBC).

Kulelewa na pamoja na chui

Wazazi wa Tiago, Leandro Silveira na Anah Jacomo ni wanabaiolojia na waratibu wa chui wa Amerika Kusini na Kati katika Taasisi ya Brazil inayosimamia ulinzi wa wanyama hao (IOP) katika jimbo la Goias.

Lengo lao kubwa ni kufanya utafiti kuhusu jinsi ya kuwahifadhi wanyama hao katika bala la Amerika.

"Mwanangu amelelewa katika mazingira ya kuishi na chui tangu alipokuwa mtoto mdogo. Bila shaka tumeweka mipaka lakini anajua tabia zao. Kwake ni jambo la kawaida," anasema Silveira, ambaye aliweka mtandaonipicha hiyo maarufu.

"Ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku,hakuna kitu cha ajabu kuhusiana na hilo."

Wazazi wa Tiago wanafanya kazi ya kuwalinda wanyama magharibi mwa Brazil

Chanzo cha picha, Family handout

Maelezo ya picha, Wazazi wa Tiago wanafanya kazi ya kuwalinda wanyama magharibi mwa Brazil

Tiago alipozaliwa wazazi wake tayari walikuwa wakiwafuga watoto watatu wa Chui.

Safari zao zilihusisha kusimama na kuwapa maziwa kwa chupa watoto wote wanne waliyoandamana nao

Kijana huyo anajihisi kuwa mwenye bahati kwa kulelewa na wanyama hao.

"Uhusiano wao ni wa upendo na kuheshimiana. Nafurahia sana kuwasaidia wazazi wangu kuwachunga wanyama hawa."

Tiago akittembea na wazazi wake na mmoja wa wanyama

Chanzo cha picha, Family album

Maelezo ya picha, Tiago amefunzwa kuweka mipaka anapowahudumia wanyama

Silveira alimfunza mtoto wake mafunzo sawa na yale yanayopewa watu wote kwa ujumla wanapokutana na duma kwa mara ya kwanza.

"Wanyama hawa waki watu kama chakula chao. Inategemea jinsi tunavyowachukulia ,kwa hivyo ni muhimu tuwaheshimu. Muonekano wao unajieleza ikiwa hawataki kukaribiwa na mtu," anasema mwanabiolojia huyo.

Mipaka

"Ni muhimu sana kuweka mipaka. Duma akitaka kukukaribia, atajileta mwenyewe. Si wanyama wanaopenda kutangamana na watu lakini wanajenga uhusiano wa maisha (na binadamu)."

Mama yake Tiago anasema hakujawahi kutokea kisa cha duma hawa kukabilina na mtoto wetu - Anah pia anasisitiza kuwa hawajawahi kumuacha mtoto wao na wanyama hao hatari peke yao.

" Tumekuwa waangalifu sana na duma hawana wanyamawengine. Tunazingatia sheria ya usalama wetu kwanza."

Tiago, mamake na mwana chui

Chanzo cha picha, Family handout

Maelezo ya picha, "nataka kuwasaidia wazazi wangu' kazi nitakapokuwa mkubwa," Tiago anasema

Hifadhi hiyo iliyo katika ardhi ya hekari 123 inamilikiwa na Silveira na Jacomo, ambao hawaruhusu watu kuwatembelea.

Lengo lao mwaka 2002 lilikuwa kuzindua kituo cha kuendesha utafiti kuhusu duma , lakini wakabadili wazo hilo baada ya kuombwa na na taasisi ya mazingira ya Brazil kuwahifadhi watoto wa duma waliyofiwa na mama zao.

Kwa mujibu wa Silveira, 95% ya shughuli za hifadhi hiyo inafadhiliwa na familia hiyo huku sehemu iliyobakia ikitokana na michango ya watu.

"Kwetu sisi hii nishghuli ya maisha ya kutafuta pesa, kwa sababu hatujawahi kupata usaidizi wa kifedha kutoka kwa umma," anasema.

The Silveira family - jaguar included

Chanzo cha picha, Family album

Maelezo ya picha, Zaidi ya wanyama 30 wamepitia animals have passed through Tiago's parents' reservation over the last decade.

Kwa sasa, familia hiyo inawahifadhi duma 14 ,ikiwa ni pamoja na watoto wanne wengine wanane wakubwa.

Katika kipindi cha mwongo mmoja uliyopita familia hiyo imewahifadhi wanyama 35.

Duma mara kwa mara wanapelekwa katika taasisi zingine ili kusaidia katika shughuli za uzalishaji na kuimarisha kizazi kijacjacho.

Duma ni moja ya wanyama waliyojumuishwa na katika orodha ya kimataifa ya wanyama waliyo katika hatari ya kuangamia duniani.

Japo kuwa wanyama hao wanapatikana katika mataifa, 21, Brazil inaaminika kuwa na karibu nusu ya idadi ya wanyama hao (20,000 hadi 30,000).

Familia ya tiago husun huwahifadhi watoto wa chui ambao mama zao wameuawa na wakulima

Chanzo cha picha, Family handout

Maelezo ya picha, Familia ya tiago husun huwahifadhi watoto wa chui ambao mama zao wameuawa na wakulima

Hata hivyo wanyama wanaoletwa katika hifadi ya IOP huregeshwa katika mbuga ya wanyama kwa kuhofia huenda wakauliwa na wakulima ambao wanalinda mifugo wao.

Sababu nyingine ni kuwa baadi ya wanyama hao wamezoena sana na wanadamu.

"Ni vigumu kwa duma hawa kuvunja uhusiano wao na wanadamu. Wakiachiliwa huenda wakajipeleka katika maeneo yaliyo na watu wakaishia kuawa na watu hao," anafafanua Jacomo.

Jaguar "akimkumbaia" Tiago

Chanzo cha picha, Family handout

Maelezo ya picha, Tiago hukutana na wanyama hao kila baada ya miezi mitatu kutokana na masomo yake

Miaka ya hivi karibuni, Tiago ametenganishwa na wanyama hao baada ya kuhamia mji mkuu wa Goiania kwa masomo yake ya shule ya upili.

Anawakosa sana chui na duma hao.

"Ni vigumu kwangu kwasababu. nimeishi nao tangu nilipokuwa mdogo. Kila wakati wazazi wangu wanapowatembelea nahisi kuwa wao pia wananikosa -wanacheza na mimi kila aina ya mchezo ,"anasema.

Picha hiyo maarufu ilipigwa Novemba 15 wakati wa moja ya ziara yake.

Kutokana na mapenzi ya sasa mvulana huyu kwa wanyama hawa, huenda siku za usoni hata wajukuu wa Silveira pia wakajenga urafiki wa karibu na wanyama hao.

"Nataka kusomea biolojia ili nami nifuate nyayo ya wazazi wangu. Wanajizatiti kuhifadhi wanyama hawa na mimi nataka kuendeleza juhudi hizo."