Unafahamu nini kuhusu vito vya Afrika vilivyoporwa na wakoloni?

Wakati wa ukoloni Afrika, maelfu ya vitu vya thamani na vya maana kubwa kitamaduni vilitwaliwa na mataifa ya magharibi na sasa vinapatikana katika makumbusho Ulaya na Marekani.

Lakini sasa, Ufaransa imezindua ripoti ambayo inatoa wito kwa turathi hizo za Afrika zilizo kwenye makumbusho nchini humo kurejeshwa Afrika. Hii imejiri huku wasimamizi wa makumbusho mengine makuu Ulaya wakisema wako tayari kuirejeshea Nigeria baadhi ya vitu vya thamani vilivyo Ulaya, lakini kwa mkopo.