Marekani: Tyson Fury na Deontay Wilder kurushiana ngumi leo

Bondia kutoka nchini Uingereza Tyson Fury anatarajia kupanda ulingoni usiku wa leo disemba mosi kupambana na mmarekani Deontay Wilder katika ukumbi wa Staples huko Los Angles Marekani.
Rekodi zinaonesha Fury mwenye miaka 30 ameshinda mapambano 27 yaliyopita huku mapambano 19 akishinda wakati mpinzani wake Wilder ameshinda mapambano 40 ambapo 39 kati ya hayo ameshinda.

Kwamujibu wa vipimo vya uzito vilivyofanyika siku ya ijumaa Fury ana uzito wa kg 116.5 wakati Wilder akiwa na kg 96.4


Taarifa zinasema kuwa Deontay Wilder ataingiza kiasi cha dola milioni 4 wakati Fury akitarajia kuondoka na dola milioni 3 za kimarekani bila kujali matokeo yatakuwaje.
Ishara za ugumu wa pambano hilo umeanza kuonekana tangu wiki iliyopita walipotaka kupigana wakati wa zoezi la utambulisho.









