Kisiwa cha Bijagos: Maji yanayotenganisha visiwa hivyo yanatumika kama kinga asili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wasafiri wanaozuru visiwa vya mbali barani Afrika vinavyofahamika kama Bijagos wanatarajia kujionea mandhari ya kipekee ya fukwe za kale na misitu asilia.
Lakini uzuri wa visiwa hivyo hauishii hapo, kwani pia vinatumika kama maabara asilia kutokana na mazingira ya kipekee ambayo yanafanyiwa utafiti wa baadhi ya magonjwa hatari ya duniani.
Mkusanyiko wa visiwa 18 kutoka pwani ya Bijagos nchini Guinea-Bissau, barani Afrika Magharibi, ni makaazi ya watu 30,000 wanaotumia lugha zao na mila za pekee.
Pia wanaishi karibu na wanyama pori na viboko wa kipekee wanaoishi katika wa maji ya bahari na kasa wakubwa.

Chanzo cha picha, Alamy
Lakini visiwa hivi vya kupendeza vinakabiliwa na magonjwa ya kila aina ambayo yanatishia maisha ya wenyeji.
Muda wa kuishi wa watu nchini Guinea-Bissau ni miaka 60, lakini katika visiwa vya Bijagos inaaminiwa kuwa chini kidogo.
Magonjwa yanayo wahangaisha watu ni pamoja na Malaria, ugonjwa wa macho unaodahamika kama trachoma, matende na minyool
Hata hivyo visiwa hivyo huenda vina siri ya kukabiliana na magonjwa hayo ipasavyo.

Maabara ya asilia
Watafiti wa matibabu wamekuwa wakifanya kazi katika visiwa vya Bijagos kwa miaka kadhaa kubaini ikiwa wanaweza kuangamiza baadhi ya magonjwa katika visiwa hivyo.
Hii ni kwa sababu visiwa hivyo vinahudumu kama maabara asilia kutokana na uhalisia wake.
Japo hali hiyo inafanya maisha ya kila siku ngumu inasaidia katika juhudi za kuangamiza magonjwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maji yanayotenganisha visiwa hivyo yanatumika kama kinga asili.
Hali hiyo inasaidia kulinganisha mbinu tofauti za kudhibiti magonjwa bila hatari ya kuharibu majaribio katika maeneo mengine ya utafiti.
Katika maeneo ya bara watu wanaweza kuingia na kutoka sehemu zinazofanyiwa majaribio ya tiba hali ambayo inafanya kuwa ngumu kubaini chanz na athari ya magonjwa hayo.
Japo kuna visiwa vingi duniani ni vichache vinakaribiana. hii inasaidia watafiti kufanya kazi tofauti lakini vikiwa mbali mbali ni bora zaidi kwa sababu uwezekano wa majaribio ya utafiti kuharibiwa ni mdogo sana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Trachoma
Watafiti kutoka chuo cha London kinachoshughulikia masuala ya usafi na tibi ya dawa za tropiki (LSHTM) awali ilikuwa inaangazi augonjwa wa macho unaofahamika kama trachoma.
Ugonjwa huo unawakabili watu milioni 1.9 dunia na ni moja ya hali ambayo inasababisha upofu unaoweza kutibiwa.
Trachoma unaweza kuambukizwa kupitia mikono iliyogusa macho ya mgonjwa, nguo zake au kupitia nzi aliyekalia jicho la mgonjwa.
Hali hiyo huwaathiri zaidi watu wanaoishi katika mazinga machafu.
Ugonjwa huo umeathiri mataifa 42 duniani.
Kuna wakati mmoja kulishuhudiwa visa ambapo kila mtoto katika vijiji vya kisiwani walikabiliwa na ugonjwa huo.

Chanzo cha picha, LSHTM
Dkt Anna Last kutoka taasisi ya LSHTM aligundua maeneo yaliyokuwa katika hatari ya ugonjwa wa trachoma kabla ya kutibu jamii nzima kwa kutumia antibayotiki ili kukomesha mzunguko wa maambukizi.
Malaria
Ugonjwa wa trachoma, ambao ni chanzo cha hali inayosababisha kupofuka macho sio tatizo pekee linalo wakabili watu.katika visiwa vya Bijagos.
Kuna magojwa mengine kadhaa ambayo yanashughulikiwa.
Kwa sasa tunaangazia ugonjwa wa Malaria ambao unasambazwa na mbu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Dalili za awali za malaria ni kuwa na homa kali kuumwa na kichwa kabla ya hali hiyo kugeuka kuwa mbaya zaidi.
Malaria huangamiza karibu watu nusu milioni duniani kila mwaka.
Ukizingatia viwango vya ugonjwa wa malaria katika visiwa hivyo - ambapo mmoja kati ya kila watu wanne wanaugua Malaria , tulibaini kuwa mbu ni wazuri sana kwa kusambaza ugonjwa huo.

Chanzo cha picha, LSHTM
Kitu cha kushangaza ni kuwa tuligundua baadhi yao hawadhuriwi na dawa ya kua wadudu.
Hii inamaanisha njia maarufu zaidi ya kudhibiti malaria ambayo ni- kutumia vyandarua vya kujikinga na mbu au kupuliza dawa ya wadudu huenda hazifanyi kazi.
Dawa mpya ya kukabiliana na mbu inatarajiwa kufanyiwa majaribio.
Tiba zilizopita zilikuwa zinalenga kukabiliana na vimelea vya malaria ndani ya mwili wa binadamu.
Lakini dawa hii mpya inalenga mbu na vimelea vya malaria ili kupunguza muda wao wa kuishi.

Chanzo cha picha, LSHTM
Katika awamu hii ya majaribio visiwa vyote vitapewa kifaa maalum cha kudhibiti viwango vya vitu kama kitanda na vyandarua vya mbu.
Katika baadhi ya visiwa pia kutatolewa dawa kama njia ya ''kukabiliana'' na zingine hazitapewa dawa.
Kundi la wenyeji wa kisiwani limepewa mafunzo ya kimatibabu, kama kutoa sampuli ya damu na kuchunguza kama ina viini vya malaria.
Pia wamejifunza jinsi ya kubaini mbu wanaosambaza malaria kwa usaidizi wa Ba, mmoja wa maafisa wa nyanjani wakitarajia kuwa wataalamu wa kwanza wa wadudu wanaofahamika kama entomologist, katika visiwa hivyo.

Chanzo cha picha, LSHTM
Matumaini ya siku zijazo
Swali la iwapo dawa hii itakomesha malaria katika visiwa hivyo linasubiri ufumbuzi.
Yote tisa kumi ni kwamba utafiti huu utawasaidi watu wanaoishi ndani na nje ya visiwa vya Bijagos.
Kila utafiti unatusaidia kujifunza mengi kuhusiana na ugonjwa wenyewe na jinsi ya kuutibu, hai ambayo inaimarisha tafiti za siku zijazo.
Utafiti unaofanywa visiwani unaweza kuendeshwa haraka zaidi kutokana na uwezo wa kudhibiti mazingira kwa ujumla.
Tunaweza kuona kile kinacho athiri eneo maalum hali ambayo inaweza kuwanufaisha watu wote kwa njia rahisi.
Mradi wa huu wa LSHTM unatarajiwa kutaendelea katika visiwa vya Bijagos kwa miaka mingine mitano.
Matokeo ya tafiti zake huenda zikatumiwa kukabiliana na magonjwa hatari kama vile malaria katika maeneo mengine.












