Moto wa nyika California: Idadi ya waliouawa yapanda hadi 25

An aerial view showing the Woolsey Fire in Malibu, California, on November 9, 2018

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Moto kwenye milima ya Malibu

Idadi ya watu waliouwa na moto ya nyika jimbo la California imeongezeka hadi watu 25.

Hii ni baada ya miili 14 zaidi kugunduliwa karibu na mji ulioteketea wa Paradise na kufikisha idadi ya vifo vilivyothibitishwa kuwa 14.

Watu wengine wawili waliuawa kusini karibu na Malibu.

Inakadiriwa kuwa watu 250,000 wamelazimika kuhama makwao kupuka mioto mitatu mikubwa katika jimbo hilo.

Rais Doanald Trump amesema kuwa usimamizi mbaya wa misitu unalaumiwa kwa moto huo.

A house on fire in Malibu, 9 November 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nyumba nyingi zimeteketea huko Malibu

Moto huu ni wa aina gani?

Moto ulianza kusambaa kwenye kaunti ya Butte siku ya Alhamisi huku na wazima moto walishindwa kuuzima moto huo ulioharibu mji wa Paradise.

Moto mwingine ulisambaa kwenda mji wa Malibu Ijumaa ambao hadi sasa umeongezeka mara dufu.

Kati ya miji ambayo kwa sasa watu wametakiwa kuhama ni pamoja na ule wa Thousand Oaks ambapo mtu mwenye silaha aliwaua watu 12 siku ya Jumatano.

Watabiri wa hali ya hewa wamenya kuwa hatari zitaendelea kushuhudiwa hadi wiki ijayo, lakini wazima moto wanasema wanajaribu kutumia hali ya utulivu wa upepo kupamba na moto huo.

Map locator
Maelezo ya picha, Ramani