Marubani wanawake: Zoom Air inaongoza kwa kuwa na marubani wengi wanawake

Mashirika ya ndege yamekuwa yakiongeza juhudi ya kuwaajiri marubani wanawake ili kufikia viwango vipya yva usafiri vinavyoendelea kuongezeka.

Mahitaji ya usafiri na utalii yameongezeka pakubwa katika miaka ya hivi karibuni huku wateja wakipendelea kujivinjra kwa mambo mapya kila uchao.

Kumekuwa na ongezeko la karibu watalii milioni 350 wa kimataifa mwaka 2017 ikilinganishwa na mwaka 2010. Kwa mujibu wa shirika la watalii duniani.

Ni shirika lipi la ndege linawaajiri marubani wengi wanawake?

Chama cha kimataifa cha marubani kinasema kuwa 5.18% ya marubani wa ndege za kibiashara ni wanawake.

Shirika la ndege la India linaajiri kiwango kikubwa cha marubani wanawake hii ikiwa ni 12.4%.

Hayo ni kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka chama cha kimataifa cha marubani wanawake(ISWAP).

Zoom Air, linalomilikiwa na shirika la ndege la India linaongoza kwa kuwa na marubani wengi wanawake.

ISWAP linasema kuwa shirika hilo linawaajiri wanawake tisa marubani kati ya marubuni 30.

Mwenyekiti wa mawasiliano katika chama cha ISWAP,Kathy McCullough, ambaye pia ni rubani mstaafu anasema ''mashirika ya ndege ya India yamekuwa yakiwashinikiza wanawake kuwa marubani wao kutokana na uhaba wa marubani''.

Ripoti iliyotolewa na Boeng imebaini kuwa ongezeko la watu wa mapato ya kadiri ,inatarajiwa kuongeza ndege za kibiashara.

Nchini Uingereza karibu 4.77% ya marubani ni wanawake

Mshahara wa marubani

Siku ya kawaida ya kazi kwa rubani huwa inajumuisha kuwasafirisha wateja au mizigo katika maeneo mbalimbali duniani.

Mshahara wa marubani wa ndege za kibiashara unategemea shirika ambalo rubani anafanyia kazi, aina ya ndege na tajiriba ya rubani.

Mshahara wa rubani anaeanza kazi ni kati ya euro elfu 20-30,000 kwa wale wanaohudumu chumba cha rubani.

Kwa marubani waliyo na tajiriba mshahara wao unaweza kufikia euro 140,000 kwa mwezi.

Mshahara wa juu zaidi unaolipwa marubani wa kikosi cha kifalme ni uero 105,250 kwa mujibu wa Utumishi wa Huduma za Taifa nchini Uingereza.

Suala la kijinsia kuhusu tofauti ya mshahara ya marubani likoje?

Mapema mwaka huu, mashirika ya Uingereza yaliyo na wafanyikazi zaidi ya 250 kwa mara ya kwanza yaliagizwa kutoa ripoti ya takwimu ya pengo la ulipaji wa mshahara kijinsia.

Shirika la ndege la Uingereza lilitajwa kuwa na mapungufu katika viwango vya ulipaji wa mshahara kijinsia.

Hali hiyo inatofautina mapato ya saa kwa wafanyakazi wote wa kiume na wa kike.

Shirika la ndege la Ryanair liliripotiwa kuwa na viwango vya juu vya pengo la ulipaji mshahara kati ya marubani wanaume na wanawake.(71.8%).

Lakini tofauti hiyo imetajwa kutokana na idadi ya marubani wa wanaume ukilinganisha na wenzao wa kike

Katika shirika la ndege la EasyJet, kwa mfano marubani ni robo ya wafanyikazi wake nchini Uingereza.

6% ya marubani wake nchini Uingereza ni wanawake- kazi ambayo inalipa euro 92,400.

69% ya wafanyikazi wanaohudumu ndani ya ndege ni wanawake na wengi wao wanalipwa mshahara wa chini unaokadiriwa kuwa euro 24,800.

Shirika hilo linasema litaweka nyongeza ya kiwango cha 20% kwa marubani wapya wa kike kufikia mwaka 2020.

Marubani wanakabiliwa na changamoto gani zingine?

  • Inachukuwa karibumiezi 18 Kupata leseni ya urubani na gharama ya kusomea urubani ni kati ya euro elfu 60-90,000.
  • Kusomea shada ya urubani inajumuisha somo la kuendesha ndege. Lakini shahada hiyo sio muhimu ukilinganisha na gharama ya kusomea urubani ambayo ni ghali mno.
  • Kufanya kiwango cha juu cha mazoezi ya urubani ukiwa mwanagenzi.