Uchaguzi Marekani 2018: Uchaguzi wa katikati ya muhula ni kama kura ya maoni kuhusu Donald Trump

Rais Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Trump akiwa katika mkutano wa kampeini jimbo la Indiana siku moja kabla ya kura ya katikati ya muhula

Wamarekani wameanza kupiga kura katika uchaguzi wa kitaifa wa katikati ya muhula ambao unaonekana kama kura ya maoni kuhusu urais wa Donald Trump.

Vituo vya kupiga kura vimefunguliwa kwenye Pwani ya Mashariki huku vyama vya Republican na Demoratic vikipania kuchukua udhibiti wa mabunge ya uwakilishi na Seneti.

Uchaguzi huu wa katikati ya muhula unakuja wakati rais Trump amefikia nusu ya muda wa uongozi wake madarakani.

Uchaguzi huo pia unatarajiwa kubaini ikiwa Trump ana uwezo wa kuongoza Marekani katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Shauku ya upigaji kura inatarajiwa kuchochea watu wengi zaidi kushiriki zoezo hilo.

wapiga kura Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Viti 435 katika bunge la waakilishi na viti 35 kati ya 100 katika Seneti vinakabiliwa na ushindani mkubwa.

Siku za hivi karibuni rais Trump amekuwa akitumia mbinu tofauti kuwasilisha hoja ambazo zinaonekana kuzua hisia mseto katika juhudi ya kuimarisha uungwaji mkono wake.

Aliyekuwa mtangulizi wake, Barack Obama - amekuwa mstari wa mbele kuendesha kampeini za chama cha Democratic - amesema "hulka ya taifaletu iko katika sanduku la upigaji kura".

Ni masuala gani muhimu katika uchaguzi huu?

Wakati wa kampeini zake za mwisho katika majimbo ya Ohio, Indiana na Missouri, bwana Trump alirejelea masuala muhimu yaliyomsaidia kushinda uchaguzi wa mwaka 2016 akisisitiza kuwa Democrats watasambaratisha uchumi na kwa kuruhusu uhuamiaji haramu.

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama

Wagombea wa Democratic kwa upande wao wameamua kujiepusha na makabiliano ya moja kwa moja na wapinzani wao na badala yake kuangazia masuala ibuka kama vile ya afya na ukosefu wa usawa katika mambo ya uchumi.

Chama hicho kunatumai kuwa wapiga kura vijana na wale wanaotokea katika makundi ya wachache waliyotengwa watavutiwa na kura hiyo kama hatua ya kupinga msimamo wa rais Trump dhidi ya masuala yanayo wagusa wao na wenzao moja kwa moja.

Trump amekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutokana na lugha yake ambayo inadaiwa kuwagawanya watu.

Upigaji kura wa mapema ulianza Novemba 4 katika majimbo ya Los Angeles na California

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Upigaji kura wa mapema ulianza Novemba 4 katika majimbo ya Los Angeles na California

Watafiti wa kura ya maoni wanabashiri kuwa Democrats huenda wakashinda viti 23 wanazohitaji kuongoza bunge la waalikilishi , na viti vingine zaidi kama 15 za ziada.

Hata hivyo Democrats wanatarajiwa kupoteza viti viwili kupoteza nafasi hiyo ambayo itawawezesha kuchukua udhibiti wa bunge la Seneti.

Nini kitakachofanyika wakati wa uchaguzi?

Baada ya miezi kadhaa ya kampeni, uvumi na mabilioni ya dola zilizotumika kwenye matangazo, wapiga kura hatimae watakuwa na nafasi ya kufanya maamuzi yao ya mwisho siku ya Jumanne.

Watu milioni 35 tayari wameshapiga kura na katika jimbo la kusini mwa Texas, idadi ya watu waliojitokeza mapema kupiga kura, tayari imepita jumla ya waliopiga kura katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Magavana pia chatachaguliwa katika majimbo 36 kati ya 50

Stacey Abrams

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Stacey Abrams anapania kuandikisha historia ya kuwa gavana wa kwanza mwanamke Marekani

Uchaguzi huu unamaanisha nini?

Uchaguzi wa katikati ya muhula utaamua ni nani atakayechukua udhibiti wa mabunge yote mawili ambayo yanatunga sheria ya nchi.

Ikiwa Republicans watafanikiwa kuendelea kuongoza mabunge ya seneti na ya uwakilishi, huenda wakaimarisha ajenda ya chama na ile ya rais Trump.

Lakini Democrats wakiwapokonya jukumu hilo huenda wakabadilisha mipango ya bwana Trump.

Katika mahojiano na runinga ya ABC siku ya Jumatatu, rais Trump alisema anataka kupunguza makali ya matamshi yake katika kipindi kilichosalia cha uongozi wake.

"Nahisi kwa kiwango fulani, sina chaguo, nadhani nilitakiwa kupunguza makali ya matamshi yangu kuanzia mwanzo."