Wanandoa wafariki kwenye ajali ya helikopta muda mfupi baada ya kufunga ndoa

Chanzo cha picha, Facebook/Bailee Ackerman
Wanandoa wachanga kutoka Texas walifariki wakati helikopta iliyokuwa ikiwasafirisha kutoka harusi yao ilianguka siku ya Jumatatu usiku kwa mujibu wa maafisa.
Will Byler na Bailee Ackerman Byler walikuwa wote wanafunzi kwenye chuo cha Sam Houston . Vifo vyao viliripotiwa kwanza na gazeti la wanafunzi.
Ajali hiyo ilitokea karibu na Uvalde karibu kilomita 135 magharibi mwa San Antonio.
Kwenye mitandao ya kijamii walioshuhudia harusi walichapisha rambi rambi kwennye mitandao ya kijamii pamoja na picha za harusi.
"Nimehusunika sana sana!" aliandika rafiki mmoja kwenye mtandao wa Facebook, akiongeza kuwa rubani wa helikopta pia naye aliuawa.
Rafiki mwingine aliondoka kwenye mtandao wa Instagram kuwa: Nina amani ndani yangu kuwa mliondoka duniani mkiwa mmejawa furaha na mapenzi. Itakuwa vyema kufanyia fungate zenu kwa Yesu.
"Tunashukuru tuliweza kuwa nanyi siku hizi chache za maisha yenu. Roho zetu zimeumia lakini tunajua hii haitakuwa daima."
Wawili hao walikuwa mume na mke kwa karibu saa moja kabla ya helikopta yao kuanguka kusini mwa Texas.
Kulinga na gazeti la nchuo the Houstonia, Will Byler aliukuwa anasomea uhandisi wa kilimo.
Bailee Ackerman Byler alikuwa akisomea mawasiliano ya kilimo. Wote walikuwa mwaka wao wa mwishoi chuoni.
Kulingana na bodi ya kitaifa ya usafiri jali hiyo ilihusu ndege ya helikopta aina ya Bell 206B.
Mabaki ya helikopta hiyo yaligunduliwa siku ya Jumapili asubuhi. Polisi walisema kulikuwa na vifo kadhaa lakini bado waliofariki hawajatajwa.
Rubani wa ndege hiyo naye pia ametambuliwa kama mmoja wa waliokufa.
Binti yake wa kambo aliiambia ABC kuwa alikuwa kampteni wa jeshi na alihudumu nchini Vietnam.












