Mabadiliko ya tabia nchi:Njia rahisi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

wind

Chanzo cha picha, Getty Images

Ongezeko la gesi ukaa kwa kiwango kikubwa kumesababishwa na shughuli za kibinadamu ,

hivi karibuni uchunguzi wa kisayansi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi umependekeza kuwa kusitisha ongezeko la gesi ukaa peke yake haitasaidia kukabiliana na ongezeko la joto kufikia nyuzi joto 1.5 au 2.

Majadiliano ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, yote yamelenga kukabiliana na gesi ukaa ili kupunguza ongezeko la joto kabla ya mwisho wa karne hii.

Mawazo haya ambayo yamekuwa yanakanganya huku wengine wanaona kama yanaingilia ukuaji wa kibiashara.

Lakini utafiti mpya kutoka kwa wanasayansi nchini Marekani,wahandisi na wataalamu wa afya umesema kwamba kuna baadhi ya njia za tekinolojia ambazo sio nzuri na ziko tayari kutumika kwa kiwango kikubwa.

1-Uoto wa asilia wa pwani

Ripoti hii inasema kwamba kuna fursa nyingi ambazo zinaweza kujitokeza kama gesi ukaa itaongezeka katika mimea na masalia katika ardhi iliyo kame au ufukweni na kando ya mito.

Kwa pamoja ardhi ya namna hiyo huwa inahifadhi kiwango kikubwa cha gesi ukaa katika mazingira yeyote.

mangroves

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mikoko usaidia kutunza gesi ukaa

Baadhi ya maeneo ya ufukweni ni miongoni mwa sehemu ya dunia ambayo imekuwa ikiathirika kila mwaka kwa hekari 340,000 mpaka 980,000.

Matatizo mengine ambayo yanaweza kujitokeza katika maeneo ya bahari duniani kote yanaweza kuharibu mazingira.

2 - Kupanda miti

miti

Chanzo cha picha, Getty Images

Kupanda miti kumeweza kuleta mafanikio chanya katika kukabiliana na gesi ukaa hivyo watafiti wanasema kwamba kupanda miti mipya kunarutubisha maeneo na tekinolojia inayotumika ni gharama ndogo ambayo inaweza kuendelea kutumika kwa sasa.

Miongoni mwa changamoto ambayo watafiti wanaeleza kuwa ni kikwazo katika wazo hili zuri la kupanda miti ni uvunwaji wa mbao, Aidha kuna ujuzi mdogo katika kupandikiza kwa miti kwa lengo la kuondoa gesi ukaa .

Karibu kila nchi inasisitiza kampeni hii ya upandaji miti ambayo ndio njia rahisi katika kukabiliana na ongezeko la gesi ukaa.

Ripoti hii inasema kuwa ni muhimu sana kama miti itaendelea kupandwa ili kuongeza rutuba katika ardhi.

3 - Utunzwaji wa misitu

forest

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Misitu ina faidia kubwa katika kutunza mazingira

Pamoja na kuongeza katika upandaji wa miti , ripoti inasema kuwa tunahitaji kutunza misitu yetu katika namna nzuri ili kuondoa gesi ukaa.

Tekinolojia inaweza kujumuisha kuongeza utunzwaji wa misitu baada misitu hiyo kusumbuliwa na moto.

Vilevile kuongeza muda wa uwepo wa misitu hiyo kabla ya kuvuna.

Hatua hii inaweza kusaidia mbao ziwe imara zaidi na kuweka vipingamizi vya miti ambayo huunguzwa.

4 - Kilimo

Ripoti hii inasema kuwa kama kutakuwa na mabadiliko ya namna ya wakulima wanavyolima na kuweza kutunza ardhi yao kwa gharama nafuu, itakuwa njia sahihi ya kuodoa gesi ukaa.

Njia hii ya upandaji mazao haihusishi mazao ya biashara.

agriculture

Chanzo cha picha, RONEMMONS

Kubadilisha namna ya kulima mazao kunaweza kurutubisha ardhi na hata masalio yake yanaweza kutengeneza nishati mbadala ambayo haiathiri mazingira.