MO Dewji: Kwa nini kutekwa kwa MO kumeacha kishindo?

Bilionea Mohammed Dewji

Chanzo cha picha, MO DEWJI

Muda wa kusoma: Dakika 4

Kutekwa kwa bilionea Mohammed Dewji, MO,kumelitikisa taifa la Tanzania na kwa kiasi dunia.

Taarifa za kutekwa, kushikiliwa na kuachiliwa huru siku tisa baadae hazikuishia tu Tanzania lakini karibu mashirika yote makubwa ya habari ulimwenguni.

Bado kuna maswali kadhaa amabayo mpaka sasa hayajapata majibu ikiwemo ni akina nani waliomvamia bilionea huyo alfajiri ya Oktoba 11 na kumuachia huru usiku wa manane wa Oktoba 20.

Kwamujibu wa maelezo ya polisi ambayo wanasema wameyapata kutoka kwa MO, 43, watekaji wake hawakuwa Watanzania. Wawili kati yao walikuwa wanongea Kingereza chenye lafudhi sawia na za nchi za kusini mwa Afrika na mmoja alikuwa akiongea kiswahili kibovu.

Ingawa Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania, Inspekta Jenerali (IGP) Simon Sirro ameapa kuwatia nguvuni wakiwa wapo hai ama wamefariki, leo ni siku ya tatu toka wamuachie Mo (na siku ya 11 toka watekeleze shambulio lao) bado hawajapatikana.

Suala la pili amabalo bado linagonga vichwa ni dhumuni la kutekwa kwa MO. Polisi pia wanasema MO aliwaeleza kuwa watekaji wake walimwambia walikuwa wakitaka pesa ndiyo wamwachie, lakini alipowapa namba ya baba yake wawasiliane naye waliogopa kufanya hihyo wakihofu kunaswa na polisi. Sirro pia alisema watekaji walimuachia MO kwa hofu ya kukamatwa baada ya uchunguzi kuimarishwa

IGP Simon Sirro
Maelezo ya picha, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameapa kuwatia nguvuni waliomteka MO.

Hata hivyo, swali linaloibuka hapa ni kuwa iwaje wahalifu ambao walijipanga ipasavyo, kwa kutumia silaha za moto, gari lenye namba za usajili za Msumbiji liloingia Tanzania Septemba mosi na kufuatilia nyendo za MO na kumteka eneo lenye ulinzi mkali walishindwa vipi kutafuta namna ya kuwasiliana na familia ya tajiri huyo ili wajipatie pesa za kikomboleo.

Ukiacha maswali hayo ambayo bado majibu yake yakipatikana yatasaidia kuelewa mkasa huu, baadi ya sababu zilizofanya mkasa huo kutikisa ni kama zifuatazo;

Utajiri wa MO

Kwamujibu wa jarida la masuala ya fedha la Forbes, MO ndiye tajiri namba moja Afrika Mashariki, na tajiri mdogo zaidi Afrika akiwa na ukwasi wa dola bilioni 1.5.

Kampuni yake ya METL, ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.

Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.

Bilionea Mohammed Dewji

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Kwa mujibu wa tovuti yake, METL inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji baiskeli.

Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Inaendesha shughuli zake Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Malawi, Msumbiji na Zambia, ambapo huajiri moja kwa moja watu zaidi ya 28,000.

Shughuli za MeTL huchagia 3.5% ya jumla ya pato la taifa (GDP) la Tanzania.

Kiwango cha wastani cha ukuaji wa mapato ya kampuni hiyo kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2014 kutoka $30 milioni hadi $1.3 bilioni kilikuwa ni 200%.

Silka ya MO

Ni ukweli kuwa kwa utajiri wake jambo lolote baya kumtokea ni habari kubwa lakini kuna upande wa pili ambao umechangia kupazwa kwa sauti zadi, nayo ni tabia yake.

MO ni tajiri wa tofauti, ukwasi alonao haukumfanya kuwa mtu wa kujikweza. Amekuwa akiishi maisha ya wazi na ya kujichanganya na watu wa kawaida.

Siku ya tukio watu wengi hususan nje ya Tanzania walikuwa wakiuliza ni kwa nini mtu wa namna yake hakuwa na walinzi ama dereva?

Bilionea Mohammed Dewji

Chanzo cha picha, MO DEWJI

Lakini kwa wamjuao, MO si mtu wa kutembea na walinzi na aghlabu huendesha mwenyewe gari yake. Polisi wanasema kuwa anamiliki silaha lakini nayo hakutembea nayo siku hiyo ya mkasa.

MO yawezekana ndiye tajiri mkubwa pekee Tanzania na Afrika Mashariki ambaye amekuwa akipanda usafiri wa kukodi wa pikipiki maarufu bodaboda.

Usafiri wa bodabda unaonekana ni wa hatari na watu wa kipato cha chini na kati. Lakini MO amekuwa akipanda kukwepa foleni sumbufu za katikati ya jiji la Dar es Salaam.

MO pia amewahi kuwa mbunge kwa miaka 10 (2005-2015) wa jimbo la Singida Mjini ambapo alikuwa kishiriki moja kwa moja katika shughuli za maendeleo na wanachi wake kama uchimbaji wa visima.

Ushabiki wa Mpira

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Watanzania wengi walianza kumjua MO mwishoni mwa miaka ya 90 na miaka ya mwanzoni ya 2000 alipojitokeza kuidhamini klabu kongwe ya mpira ya Simba.

Watanzania waliowengi wamegawanyika katika kuzishangilia klabu kongwe mbili za Simba na Yanga hivyo kuongoza na kufadhili klabu hizo lazima utapata umaarufu.

Kwa sasa MO ni muwekezaji mkuu ndani ya klabu ya Simba na anamiliki hisa 49%.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Visa vya utekaji

Baada ya kutekwa kwa MO Waziri wa mambo ya Ndani Tanzania Kangi Lugola alijitokeza na kusema kuna hofu kwa Watanzania juu ya matukio ya kutekwa na akasemaa hofu hiyo inabidi iondolewe.

Kwa mwaka 2018 alisema visa 21 vya watu kutekwa viliripotiwa na kati ya hivyo watu 17 walipatikana salama.

Hata hivyo kwa miaka ya karibuni nchini Tanzania kutekwa, kuchukuliwa ama kushambuliwa na watu wasiojulikana kumekuwa ni hali ya kutisha.

MO amekuwa tajiri wa kwanza kutekwa na watu wasiojulikana.

Hata hivyo, idadi ya visa vilivyotekelezwa na wasiojulikana Tanzania ni vingi.

Matukio vya watu wasiojulikana

  • Mauaji ya Kibiti mwaka 2017: Viongozi wa CCM, askari zaidi ya 10 na wananchi karibu 40 katika eneo la Kibiti walishambuliwa na kuuawa na watu wasiojulikana.
  • 11 Februari, 2018 Kiongozi wa Chadema Daniel John alitekwa na kisha aliuwawa kikatili wakati wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni. Mwili wake ulipatikana mnamo 14 Februari.
  • Aprili 2017, Mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzie wawili watekwa na watu wasiojulikana na kuachiwa baada ya siku 3.
  • Mnamo 7 Septemba, 2017, Mnadhimu Mkuu wa upinzani bungeni, mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Area D Mkoani Dodoma. Bw Lissu pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika.
  • 21 Novemba, 2017 Mwandishi wa habari wa Mwananchi Communications Limited Azory Gwanda alipotea katika mazingira ya kutatanisha na mpaka sasa hajapatikana.
  • Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Ben Saanane alipotea katika mazingira ya kutatanisha.