Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mgahawa ambapo wateja hulipa kwa Bitcoin na kufunzwa kuhusu sarafu hiyo Kenya
Katika maeneo ya mlima Kenya upo mgahawa mmoja unaotumia teknollojia malipo ya sarafu ya dijitali maarufu kama Bitcoin.
Mgahawa wa Betty's Place, ni maarufu kwa nyama choma, ambacho ni chakula kinachopendwa sana na Wakenya.
Mgahagwa huu ulio mji wa Nyeri umbali wa kilomita 150 kutoka mjini wa Nairobi, ni kati ya biashara chache nchini Kenya zinazoruhusu wateja kulipa kwa kutumia mifumo miwili ikiwemo ya Bitcoin na Dash.
"Kwa kuwa sasa dunia imekuwa ya kidijitali, mgahawa wangu nao pia unaendelea kuwa wa kidigitali," anasema Beatrice Wambugu, mmiliki wa mgahawa huo.
"Ninawavutia wateja tofauti kutoka sehemu tofauti za dunia, sarafu yoyote wako nayo, kama inakubalika sisi tunaikubali pia."
Bi Wambugu alianza kufanya biashara ya Bitcoin miaka wiwili uliyopita na kwa mwaka moja alipata pesa za kununua hoteli ya ghorofa mbili mjini Nyeri na kuiita Betty's Place.
Mafunzo ya Bitcoin
Betty's Place sio tu mahala pa maankuli lakini imekuwa eneo la kuwavutia watu ambao wanataka kufahamu zaidi kuhusu sarafu ya kidijitali.
Wakati inapowadia kuitumia teknolojia mpya, Bi Wambugu anajieleza kuwa mfumbuzi wa sarafu ya kidijitali.
- Bitcoin ni nini? Ni sarafu ya kidijitali isiyo na noti wala sarafu. Ni ya dijitali na iko tu kwenye mitandao na wala haitolewi na serikali wala benki.
Malipo kwa njia ya Bitcoin yamekuwa mazuri - karibu shilingi 30,000 za Kenya au dola 300 kutoka kwa karibu watu 20.
Ili kuwezesha watu zaidi kushiriki, yeye hufunza watu jinsi ya kufanya biashara ya Bitcoin kila Jumapili kwenye mgahawa wake.
"Nimetenga siku moja ambapo mimi huwafunza wateja. Yeyote yule anayeweza kuuliza kuhusu sarafu ya dijitali, vile hufanya kazi, mimi huwafunza," Anasema
Simu za mkononi hurahisisha malipo ya sarafu ya kidijitali katika Betty's Place na kwa wafanyabiashara wengine.
Barani Afrika simu imekuwa kifaa muhimu cha kubadilisha jinsi watu hufanya biashara, na ukuaji wa sarafu za Bitcoin huenda siku moja ukawa mshindani mkubwa wa mifumo kama M-Pesa kama njia mwafaka ya malipo.
Kuna wale wamepoteza
Peter Oduba ambaye angekuwa mwekezaji kutoka Kenya, alijipata kwenye kile kinatajwa kuwa Bitcoin Ponzi scam au Crypto Wealth ambapo alipoteza pesa nyingi.
Aliiambia BBC kuwa ulaghai huo ulihusu kile kilitajwa kuwa viungu sita vya wawekezji kuingia.
"Chungu cha kwanza ukishaingia unaleta watu wawili, kisha watu hao wawili wanawaleta wengine wawili," alieleza.
"Mara watu wengine wawili wanapowaleta wengine sasa unaweza kuwa na karibu na watu saba au nane, ikimaanisha kuwa mara unapokuwa na watu saba mtu ni lazima aruke chungu cha pili.
"Walikuwa wanasema mara unaporuka kwenda chungu cha pili watakupa pesa kwa njia ya Bitcoin. Hatukujua ulikuwa ni ulaghai, na tukafanya hivyo kwa muda mrefu na mara ikaporomoka."
'Sarafu ya kidijitali ji kamari'
Benki kuu nchini Afrika Kusini ilibuni mfumo mapema mwaka huu unaojulikana kama Project Khokha, uliotumia teknolojia ya Blockchain kuwezesha malipo ya benki.
Ilingunduliwa kuwa malipo yanaweza kufanyika chini ya masaa mawili na uhakika wote na malipo ukjwepo.
Nchini Nigeria nyumbani kwa soko kubwa zaidi la Bitcoin barani Afrika ambapo dola milioni 4 hubadilishwa kila siku, wale wanadhibiti wamechukua msimamo mkali kuliko wenzao wa Afrika Kusini.
Mapema mwaka huu bunge la senate liliamrisha kufanyika uchunguzi kuhusu Bitcoin na gavana wa benki kuu Godwin Emefiele alionya: Sarafu ya kidijitali au Bitcoin ni kamari na kuna sababu ya kila mtu kuwa makini.