Ebola: WHO lasema hakuna dharura ya kimataifa

Chanzo cha picha, John Wessels/Oxfam
Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini humo bado hauhitaji jitihada za dharura za kimataifa huku likisisitiza kuwa linaufuatilia kwa karibu sana ugonjwa huo.
Kauli hii inakuja baada ya mkutano maalumu wa dharura uliofanyika mjini Geneva kujadili hali ya ugonjwa huu nchini DRC.
Kauli ya mwisho iliyokubalika katika kikao hicho ni kwamba hatua zinahitaji kushinikizwa katika kupambana na ugonjwa huo hatari.
Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani kusini zimetakiwa kuchukua tahadhari ya haraka kutokana na kusambaa kwa ugonjwa huu, kwasababu hali inaweza kubadilika wakati wowote kuanzia sasa.
Kumeshuhudiwa ongezeko la visa vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na mzozo unaoendelea, Kupoteza imani kwa jamii katika maeneo yalioathirika, yote haya yanatatiza jitihada za kudhibiti ugonjwa huo.
Mapigano katika eneo hilo yanafanya kuwa vigumu kudhibiti ugonjwa huo.


Rwanda, Burundi Uganda katika hatari kubwa:
Huenda hakuna hatari ya kimataifa, lakini shirika la afya duniani linasema hatari ni kubwa kwa : Uganda, Rwanda, Burundi na Kudan Kusini na mataifa yanmeambiwa yajitayarishe.
Lakini ina maana gani katika suala la hatua zinazostahili kuchukuliwa? Na je mataifa hayo yamefanya nini kufikia sasa?
Uganda:
Dkt Yonas Woldemariam. mwakilishi wa WHO nchini Uganda ameielezea BBC kwamba anaamni kwamba taifa hilo limejitayarisha lakini hilo anasema halipaswi kuwazuia kuwana wasiwasi.
Kufikia sasa wanasema kuna mfumo mzuri wa utaratibu unaoongozwa na wizara ya afya nchini, na wametuma maafisa wa kutosha kutoka WHO na washirika wengine.
Tathimni za kitaifa na kieneo zimekuwa zikifanyika kila wiki na kuikagua hali na kuangalia kiwango cha utayari kinachohitajika.
Ameeleza kwa mfano wamekuwa wakichunguza uvukaji mipakani uko vipi, ukaguzi wa wageni uko vipi, uhamaisho katika jamii na maafisa wa afya, na je jamii ina njia za kuwasilisha tahadhari iwappo kuna tukio lolote la kutia shaka.
Akizungumza kutoka eneo la mpakani na DRC, Yonas amesema licha ya hayo bado ni lazima yote hayo yashinikizwe, na kuongezwa nguvu na kuhakikisha washirika wote wanachangia katika hilo.

Chanzo cha picha, John Wessels/Oxfam
Rwanda:
Wizara ya Afya imetoa hakikisho kwamba serikali imejitayarisha vilivyo na iko tayari kuzuia uwezekano wowote wa kuzuka maambukizi ya Ebola.
Tayari ukaguzi wa wasafiri wanaoingia nchini umekuwa ukifanyika, kufuatia kuzuka kwa mlipuko huo nchini DRC.
Lengo ikiwa ni kuhakikisha kuwa kisa chochote cha Ebola kinaweza kutambuliwa na mhusika kutengwa.
Wasafiri au wageni wanaoingia, hupimwa joto la mwili na kuulizwa historia ya safari walizofunga, na pia huchunguzwa kwa dalili nyingine zozote za homa hiyo inayotokana na virusi vya Ebola.
Kwa sasa tahadhari imetolewa kwa wananchi kutosafiri kwenda katika maeneo yalioathirika na kuripoti dalili zozote wanazozishuku.
Burundi:
Burundi inaonekana kuwa katika hatari zaidi kutokana na kuingia na kutoka kwa watu mpakani kutoka matifa ya Rwanda na Uganda.
Wizara ya afya imeeleza kwamba tayari kuna vifaa vya kukabiliana na janga iwapo litatokea.
Imesititiza umuhimu wa mawasailiano na uhamasisho wa umma ili wajue mapema dalili na namna wanaweza kuzuia virusi vya ugonjwa huo hatari.
Kumeidhinishwa kampeni za uhamisho kwa wahudumu wa afya.
Tangu kuzuka kwa janga la Ebola Burundi haijakuwa na uwezo wa kufanya majaribio ya sampuli kubaini virusi vya Ebola na imekuwa ikipeleka sampuli hizo nchini Uganda kwa uhakikisho.

Chanzo cha picha, John Wessels/Oxfam
Sudan Kusini:
Sudan kusini ni nchi nyingine ilio katika hatari kubwana iliopawa uzito na shirika hilo la WHO.
Ni katika kushinikiza utayari kutokana na ukaribu wa taifa hilo na eneo ambalo mlipujko wa Ebola umetokea.
Shirika la afya duniani WHO linasema taifa hilo changa barani Afrika limeongeza shughuli za matayrisho.
Wizara ya afya kwa ushirikiano wa WHO, Kituo cha udhibiti wa magonjwa (CDC) na washirika wengine imejishughulisha na kuidhinisha hatua za muitikio.
Hii ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa vikosi katika idara mbalimbali na viwango mbalimbali, uhamasisho na viongozi wakuu kitaifa, washirika na washirika wa kutoa misaada.

Takwimu kutokana na mlipuko uliopo sasa wa Ebola nchini DRC, unaonyesha kwamba kati ya watu 10 walioambukizwa Ebola 6 hufariki.
Hivyo basi kutokana na kukithiri kwa virusi hivyo, mkondo wa sasa wa maambukizi, na mifumo dhaifu ya afya nchini humo na hata Sudan kusini, ni muhimu kuimarisha uwezo wa kitaifa ili kujitayarisha na kuitikia vilivyo hususan katika maenoe maalum ya kuiweza kuingia kwa Ebola.














