Unapotea njia kila wakati: Vidokezo hivi vitakusaidia kuimarisha kumbukumbu yako

Ramani na Dira

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ramani na Dira

Je umekua na tatizo la kuenda kutoka sehemu moja hadi nyingine, ukajipata mahali pengine tofauti kabisa badala ya kule ulikotarajia kuenda?

Ama ukajipata unazunguka pale pale ulipokua ukisema "Sijapotea , nimechanganyikiwa tu"?

Kama jibulako ni ndio, Vidokezo hivi kutoka kwa Catherine Loveday, mtaalamu wa saikolojia wa neva vitakusaidia

1. Jiandae kimawazo

Muonekano wa Les Rambles, barabara kuu mjini Barcelona, Catalonia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muonekano wa Les Rambles, barabara kuu mjini Barcelona, Catalonia

Fanya utafiti wa muonekano wa mahali unakoenda.

2. Makinika

Msafiri akijaribu kusoma ramani ya mji wa London

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni rahisi sana usipoteze muda wako kujipatia usumbufu wa akili

Jaribu kumakinika- Hali hiyo itakusaidi kutulia kwa sababu ukiwa na wasiwasi utapoteza uwezo wako wa kukumbuka.

3. Elekeza mawazo yako kwa kitu kimoja

Wapenzi wakijaribu kutafuta mahali wanakoenda

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wapenzi wakijaribu kutafuta mahali wanakoenda kwa kutumia kifaa maalum

Kuzungumza kwa simu, kutuma ujumbe au kufikiria vitu vingine kutaathiri kumbu kumbu yako ya mahali ulipo.

4. Weka alama Jengo au mnara wa kihistoria

Eneo maarufu mjini Istanbul, Uturuki wakati wa jioni

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eneo maarufu mjini Istanbul, Uturuki wakati wa jioni

Jaribu kutafakari muonekano wa kitu maalum iwe ni jengo kubwa mnara au bango katika eneo unalozuru.

Ukiwa katika mji huo huenda kuna jengo ambalo unaweza kuona urefu wake kutoka kila pembe ya mji.

Jengo kama hilo litaimarisha kumbu kumbu yako.

5. Angalia nyuma yako

Mwanamke akiangalia kituo cha treni

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nitakumbuka mahali hapa tena?

Mara nyingi watu huzingatia wanakoenda lakini wale wanaoangalia nyuma walikotoka huwa na uwezo wa kukumbuka walichoona hasa wakati wa kurudi.

6. Kumbuka yale kile ulichokua unafanya ukiwa njiani

Picha ya kompyuta inayo onyesha mfumo wa ubongo na kumbukumbu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya kompyuta inayo onyesha mfumo wa ubongo na kumbukumbu

Hii itakusaidia ukiamua kurudi nyuma wakati umepotea.

7. Piga picha

Mwanamke wa kijapan akitembea kijijini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamke wa kijapani akitembea kijijini

Unaweza pia kupiga picha vituo maalum ambayo itakusaidia kukumbuka ulipokua wakati wa safari ya kurudi.

Utafiti umebaini kuwa picha ni bora zaidi kuliko kurekodi kanda ya video.

8. Jaribu kutathmini safari yako

Kuimarisha ramani ya akili humfanya mtu kuwa mkakamavu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuimarisha ramani ya akili humfanya mtu kuwa mkakamavu

Kumbuka kile ulichofanya tangu ulipoanza safari.

Hatua hiyo itakusidia kuimarisha kumbu kumbu yako.

Ikiwa bado unajikuta ukiwa na tatizo la kusahau unakoelekea, unaweza kutumia huduma ya GPS, katika simu yako lakini ni vyema zaidi kutumia natumia kumbu kumbu yako ya asili.

Picha zote zina hakimiliki