Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Unapotea njia kila wakati: Vidokezo hivi vitakusaidia kuimarisha kumbukumbu yako
Je umekua na tatizo la kuenda kutoka sehemu moja hadi nyingine, ukajipata mahali pengine tofauti kabisa badala ya kule ulikotarajia kuenda?
Ama ukajipata unazunguka pale pale ulipokua ukisema "Sijapotea , nimechanganyikiwa tu"?
Kama jibulako ni ndio, Vidokezo hivi kutoka kwa Catherine Loveday, mtaalamu wa saikolojia wa neva vitakusaidia
1. Jiandae kimawazo
Fanya utafiti wa muonekano wa mahali unakoenda.
2. Makinika
Jaribu kumakinika- Hali hiyo itakusaidi kutulia kwa sababu ukiwa na wasiwasi utapoteza uwezo wako wa kukumbuka.
3. Elekeza mawazo yako kwa kitu kimoja
Kuzungumza kwa simu, kutuma ujumbe au kufikiria vitu vingine kutaathiri kumbu kumbu yako ya mahali ulipo.
4. Weka alama Jengo au mnara wa kihistoria
Jaribu kutafakari muonekano wa kitu maalum iwe ni jengo kubwa mnara au bango katika eneo unalozuru.
Ukiwa katika mji huo huenda kuna jengo ambalo unaweza kuona urefu wake kutoka kila pembe ya mji.
Jengo kama hilo litaimarisha kumbu kumbu yako.
5. Angalia nyuma yako
Mara nyingi watu huzingatia wanakoenda lakini wale wanaoangalia nyuma walikotoka huwa na uwezo wa kukumbuka walichoona hasa wakati wa kurudi.
6. Kumbuka yale kile ulichokua unafanya ukiwa njiani
Hii itakusaidia ukiamua kurudi nyuma wakati umepotea.
7. Piga picha
Unaweza pia kupiga picha vituo maalum ambayo itakusaidia kukumbuka ulipokua wakati wa safari ya kurudi.
Utafiti umebaini kuwa picha ni bora zaidi kuliko kurekodi kanda ya video.
8. Jaribu kutathmini safari yako
Kumbuka kile ulichofanya tangu ulipoanza safari.
Hatua hiyo itakusidia kuimarisha kumbu kumbu yako.
Ikiwa bado unajikuta ukiwa na tatizo la kusahau unakoelekea, unaweza kutumia huduma ya GPS, katika simu yako lakini ni vyema zaidi kutumia natumia kumbu kumbu yako ya asili.
Picha zote zina hakimiliki