Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Serikali ya Uganda yawaagiza wakaazi wa Bududa wahame kuepuka maporomoko ya ardhi
Serikali ya Uganda imewataka watu wa wilaya ya Bududa mashariki mwa Uganda wahame kutoka kijiji cha Bukalasi na vijiji vyengine vilivyoko kwenye wilaya ya Bududa kutokana na maporomoko ya mawe.
Mvua kubwa ilionyesha siku ya Alhamisi iliopita ilisababisha uharibifu wa majumba mengi na kusababisha vifo vya watu takriban 50 huku miili ikiendelea kupatikana.
Kuna hofu ya kutokea maradhi ya kuambukiza kutokana na maiti zinazo patikana katika Mto Sume na mto Manafwa baada ya mvua hiyo kubwa.
Rais Yoweri M7 amewafariji na kuwapa pole wakaazi wa wilaya hiyo ya Bududa wanaofikia 250,000 na amesema atawapa Sh Million 5 za Uganda kila familia iliopoteza mtu wake na Sh Miilion 2 kwa kila aliejeruhiwa .
Wakaazi wengi wa Wilaya ya Bududa wanaonekana sasa kukubaliana na mpango wa Serikali licha ya baadhi kuitaka serikali iwahakikishie zoezi hilo litafanyika.
Hata hivyo rais Museveni amewambia watu wa Wilaya ya Bududa njia peke sasa nikuwahamisha watu wote kutoka eneo la Bududa.
Serikali ya Uganda tayari imeweza kuhamisha familia za watu zaidi ya 600 na kuwapa ardhi ya kukaa na kulima na pia Waziri Mkuu Ruhakana Rugunda amesema serikali imetumia Sh Billion 8 kununua ardhi nyengine eneo la Bulambuli.
Serikali sasa inafanya mipango hatua kwa hatua kuanza kuwahamisha watu wote kutoka wilaya ya Bududa rasili mali zitakapo patikana .
Sir Bob Moshikori Mfalme wa Masaba eneo la Bugisu ameitaka serikali na watu wote wa kabila la masaba walioko Uganda na hata walioko nchini Kenya wote wajitokeze kwa hali na mali kuwasaidia ndugu zao wa wilaya ya Bududa Mfalme alikozaliwa.
Baadhi ya watu waliohamishwa na kupelekwa eneo la Kiryandongo 2010 wamekua wakilalamika kuhusu ugumu wa maisha huko na hali wengine wamekatazwa kuishi Kiryandongo kwa sababu hawajulikani katika ofisi kuu ya waziri mkuu wa Uganda.
Mzee Patrick Namukobe alipoteza watoto 6 katika maafa ya mwaka 2010 na bado anauchungu sana serikali kushindwa kuwahamisha na kuwapeleka Bulambuli, lawama nyingi akiwatupia baadhi ya wabunge wa eneo hilo .
Diwani wa wilaya ya Bukalasi Shibale Milton lilopoteza watu wengi kwenye maafa ya Alhamisi, amesema walikubali kuondoka Bududa tangu mwaka 2010 watu walipo fariki eneo la Namutsi lakini amesema wanasiasa ndio wamekua wakikwamisha zoezi la kuwahamisha.
Eneo la Bududa Kimazingira likoje?
- Bududa ni bonde liloko chini ya Mlima Elgon wanao uiita Mama.
- Mji huo unapatikana ndani ya mbuga ya kitaifa ya Mlimat Elgon
- Bududa upo 4,300 ft juu ya kina cha bahari.
- Kumewahi kutokea maporomoko ya ardhi mnamo Machi mosi 2010.
- Yalitokana na mvua kubwa ilionyesha kati yasaa sita na saa moja usiku.
- Inaaminika takriban watu 100 waliuawa na miili ya watu 94 ilipatikana.
- Eneo hilo linafahamika kwa ukulima wa kahawa.
- Hali ya hewa katika eneo hilo kwa kawaida husababisha ukavu katikati ya vipindi vya mvua.
- Serikali inataja kwamba chanzo kikuu cha hali hiyo ni ukataji miti inayomea katika mlima juu ya upande wa kuteleza.
- Kwa kawaida ukataji misitu katika enoe la milimani husababisha maporomoko ya ardhi.
Kwa sasa kinacho subiria ni lini Serikali ya Uganda itaanza zowezi la kuwahamisha watu wote huku idadi ya waliofariki ikiwa imefikia takriban 50 na watu wengine kadhaa wakiwa bado hawajulikani walipo .
Zoezi la kuwatafuta manusura na waliofariki bado linaendelea hadi pale serikali itakapo tangaza rasmi kukomeshwa kwa zoezi hilo .