Kujivunia wafanyakazi wa msaada wanaojitolea

Chanzo cha picha, Marcus Perkins
Maisha ya wafanyikazi wa kutoa misaada katika maeneo ya vita sio rahisi kama mnajuavyojua, anasema mwandishi wa zamani wa BBC Mark Doyle.
Kwa sasa Doyle ambaye anahudumu katika sekta ya utoaji misaada, ameamua kuelezea maisha ya kila siku ya wafanyikazi wa kutoa misaada nchini Zambia.
Wanaume unaowaona happo juu kwenye picha huenda wasikupatie taswira kamili ya hali ya wafanyikazi wa kutoa misaada barani Afrika.
Picha za kawaida ambayo watu wamezoea kuona ni ya muuguzi akimhudumia mtoto mgonjwa, na muuguzi huyo huenda anatoka mataifa ya bara ulaya.
Hata hivyo idadi kubwa ya watu amabo wanaendesha miradi ya misaada barani Afrika ni Waafrika wenyewe.
Kazi yao kubwa ni ya kuhakikisha msaada inawafikia watu vijijini katika maeneo ambayo barabara ni mbovu au wakaazi wamezingirwa na maji ya mafuriko.
Kukabiliana na moto
Kiongozi wao Robert Ntitima alikua anakaribia kukamilisha safari ya 700km sawa na (maili 435) kutoka mji mku wa Zambia, Lusaka, hadi kijiji Malumba magharibi mwa nchi.
Alikuwa anampeleka mtaalamu wa macho kumfanyia upasuaji mgonjwa aliyepofuka macho baada ya gari lake kukwama ndani ya mchanga.
Giza lilipoanza kuingia, moto aliyowakishwa na mkulima mmoja kuchoma kichaka katika shamba lake ulimshinda nguvu na kuanza kuja kwa gari lao.
Moto huo ulitishia kuchoma na kulipua gari lao iwa mafuta yangelishika moto.
Bwana Ntitima na dereva wake Clinton Bakala hawakua na budi bali kukabiliana na moto huo kwa kutumia majani mabichi huku waking'ang'ana kutoa gari lao lililokua limekwama kwa matope.
Baadaye cheini ya gari lingine ilitumiwa kuivuta na kulitoa gari hilo kutoka kwa mchanga.

Chanzo cha picha, Uniting to Combat NTDs
Ahadi kwa mwanawe
Baada ya kufanikiwa kutoa gari lao kwa mchanga, bwana Ntitima alichukua muda kupigia simu familia yake kabla ya kuendelea na safari.
Ilikua siku ya kuzaliwa ya mtoto wake Sally Mika ambaye alikua anatimiza wa miaka minne.
Aliahidi kuuwa atamfanyia sherehe atakaporudi nyumbani.
Hii nsio taswira ya maisha ya kila siku ya wafanyikazi wa kutoa misaada katika eneo la magharibi mwa Zambia.
Awali gari lililokua limembeba mtaalamu wa macho, Bruno Kandei, lilikwama ndani ya maji ya mafuriko yaliyokua yameziba sehemu ya barabara.
Daktari Kandei ni mtaalamu wa kutibu ugonjwa wa trachoma, ambao ni chanzo cha hali inayosababisha kupofuka ambako kunaweza kuepikika duniani.
Kwa sasa anafanya kazi kwa niaba ya shirika la kimataifa la misaada la linalofahamika kama Sightsavers.
Kando na utaalamu wake wa macho, alilazimika kuwa mtaalamu wa kutoa gari lililokwama ndani ya maji ya matope.
"Bruno" ni jina la utani. Rafiki yake wa tangu miaka ya 1980 alilipata kutoka kwa mwingereza schoolteacher ambaye alikuwa anafanya kazi mjini Kalabo Zambia.
Kijana huyo na mwalimu Brunowalikuwa wachezaji mpira. Jina "Bruno" limepewa wazambia wengi.

Chanzo cha picha, Uniting to Combat NTDs
Jina halisi la Daktari Kandei lilikua "Kubona".
Daktari Kandei, 53, anaeleza maana ya jina lake."Kwa lugha yetu 'Kubona' inamaanisha 'uwezo wa kuona,'"
"Pengine jina langu lilikua mpango wa Mungu kunionyesha kuwa nitawatibu watu walio na tatizo la kuona."
Bada ya safari ya siku mbili ,bwana Ntitima na Daktari hatimae walifika katika kliniki ndogo ambako wagonjwa walikua wanawasubiri.
Magari yaliyokua yamebeba wagonjwa pia yalikwama barabarani mara kadhaa.
Lakini kila mmja wao alijtahidi kufika ili apate kuhudumiwa amefika.
Karibu watu milioni 158 duniani wameathiriwa na trachoma
Utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa karibu watu milioni 158 kote duniani wanakabiliwa na hatari ya kuugua ugonjwa wa trachoma ambao husababisha upofu
Nusu ya hao watu milioni 158 wanatibiwa kwa kutumia antibayotiki lakini hiyo pekeee haitoshi maana kuna mengi yanahitajika.

Chanzo cha picha, Uniting to Combat NTDs
Trachoma ni moja ya magonjwa ya tropiki yaliyotelekezwa ambayo huwaathiri watu masikini katika jamii.
Magonjwa mengine ni kama minyoo na ugonjwa wa malale.
Magonjwa haya yanapuuzwa kwa sababu haya hitaji matibabu ya dharura kama vile kukabiliana na homa hatari ya ebola.
Kwa wazee trachoma husababishwa na kumea kwa kope za macho ambazo huingia machoni.
Muathiriwa anahisi maumivu makali na hatimae kupofuka asipotibiwa mapema.
Trachoma nini?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Trachoma ni ugonjwa unaosababisha mtu kukosa uwezo wa kuona
- Husababishwa na viini vinavyojulikana kama Chlamydia trachomatis
- Dalili zake ni pamoja na kupungua kwa nguvu za kuona vizuri, kuumwa na kuwashwa na macho.
- Mtu huambukizwa kwa kugusa kwa mikono jicho au pua ya mtuaanayeugua ugonjwa huo au kutumia tauli, nguo yake. Nzi pia huambukiza
- Hutibiwa kwa kutumia antibaotiki au kufanyiwa upasuaji.
- Trachoma husababisha upofu ambao hauwezi kutibika
Wataalamu wanasema tiba ya trachoma njia ya upasuaji inachukua dakika 20 .
Inahusisha kurudisha kope ya mgonjwa katika nafasi yake.
Kwa kutumia dawa ya kufisha ganzi, bi Simate alikua akiongea na daktari hadi alipokamilisha shughuli ya upasuaji.
Hakuna umeme
Daktari Kandei alifanya upasuaji wa nann ahiyo kwa wagonjwa wengi hadi giza lilipoingia na kumlazimu kusitisha shughuli hiyo.
Hii ni kwa sababu umeme haujafika vijijini.

Chanzo cha picha, Robert Ntitima
Yeye na wenzake husafiri vijijini kila baada ya wiki mbili ili kuwahudumia wagonjwa ambao hawana uwezo wa kuja mjini kwa hospitali kuu.
Bwana Ntitima alirudi salama mjini Lusaka,na kumuandalia sherehe ya siku ya kuzaliwa Sally Mika kama alivyoahidi.













