Hukumu ya Kifo: Ni nchi ngapi bado zinatekeleza adhabu za kifo?

Antonio Guterres, UN secretary general

Chanzo cha picha, Getty Images

Madai: Inadaiwa kuwa inawezekana mataifa 170 wameachana na adhabu hiyo ya kifo au wameanzisha mbadala wa adhabu hiyo.

Hukumu: Kwa mujibu wa Amnesty International mwaka 2017, nchi 142 wameacha kutoa hukumu ya kifo kisheria na kiutekelezaji.

Short presentational grey line

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo na kusifia jitihada ambazo mataifa mbalimbali wamezichukua ili kutokomeza adhabu hiyo.

Alisema "mataifa 170 inawezekana wameacha kutoa hukumu ya kifo au wameanzisha mbadala wa adhabu hiyo.

Je amesema kweli?

Makubaliano ya kusitisha sera au utekelezaji

Ripoti ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu hukumu ya kifo imewasilishwa katika tume ya haki za binadamu mwezi Septemba mwaka huu na kusema kuwa kuna mataifa 170 wameachana na adhabu hiyo ya kifo kisheria na utekelezaji au hajauliwa mtu kwa zaidi ya miaka 10.

Umoja wa mataifa ambayo ina wanachama 193, hivyo ni mataifa 23 tu ndio ambayo inawezekana walitoa hata hukumu moja ya kifo katika muongo uliopita.

Umoja wa mataifa unasema pia kuwa takwimu hizo zinajumuisha taarifa ambazo wamezipata kutoka nchi wanachama pamoja na asasi za kiraia.

hukumu ya kifo duniani

Hata hivyo ,Amnesty inasema kuwa ni mataifa 142 ambayo inawezekana kuwa wameachana na hukumu ya kifo na ndani ya miaka mitano iliyopita, mataifa 33 wametekeleza hukumu hiyo ya kifo hata kwa mtu mmoja.

Amnesty inakusanya takwimu zake kwa kutumia takwimu rasmi, ripoti za vyombo vya habari na taarifa zilizotolewa kutoka kwa watu waliohukumiwa kifo na familia zao na wawakilishi.

Nchi nne zilitekeleza mauaji kwa asilimia 84 mwaka 2017(Saudi Arabia, Iraq, Pakistan na Iran). Idadi hiyo haijajumuisha China ambapo takwimu zake ni siri ya taifa hilo. Amnesty inakadiriwa kutoa hukumu ya kifo kwa maelfu ya watu kila mwaka.

Njia ambazo zimetumika kutekeleza adhabu hiyo mwaka 2017 ilikuwa ni pamoja na kupigwa, kunyongwa, kuchomwa sindano na kupigwa risasi.

Shirika la haki za binadamu imerikodi idadi ya hukumu ya vifo 2,591 katika nchi 53 katika mwaka 2017.Lakini katika baadhi nchi, kesi hizo za hukumu hizo za kifo huwa zinabadilishiwa adhabu labda kwa mtu kuwekwa miaka mingi gerezani.

Kwa mujibu wa Amnesty:

  • Nchi 106 hukumu ya kifo haikubaliki kisheria
  • Nchi 7 zinaruhusu hukumu ya kifo lakini kwa uhalifu mkubwa ambapo pia huwa inategemea na mazingira yenyewe kama wale ambao waliofanya uhalifu wakati wa vita.
  • Nchi 29 ambazo sheria yao inaruhusu adhabu ya kifo lakini hakuna aliyeuliwa takribani miaka 10 na hazaijasema rasmi kuwa zitaachana na adhabu hiyo au kuwa na sera inayopinga
  • Nchi 56 ambazo zinatekeleza hukumu ya kifo na sheria na mamlaka hayajaweka tamko rasmi ya kuachana na adhabu hiyo

(Amnesty imejumuisha nchi tano ambazo sio nchi wanachama wa Umoja wa mataifa).

ramani

Serikali ya Malaysia imetangaza kuwa na nia ya kuachana na hukumu hiyo ya kifo.

Takribani watu 1,200 ambao wanadhaniwa kuhukumiwa kifo nchini Malasia, ambapo hukumu hiyo hutolewa kwa mashtaka kama mauaji, na usafirishaji wa madawa ya kulevya. Bunge litawapa kipaumbele suala hili katika mswada ambao utakuepo kipindi kijacho.

Kama Malaysia itaachana na hukumu ya kifo, itajumuika na Guinea na Mongolia ambazo ziliachana na adhabu hiyo mwaka 2017.Rais wa Gambia Adama Barrow alitangaza kuachana na adhabu hiyo mwanzoni mwa mwaka huu na huku ikiripotiwa kuwa hukumu ya kifo kutekelezwa nchini Gambia ilikuwa mwaka 2012.

Mwezi June, bunge la , Burkina Faso imeanzisha adhabu mpya ambayo itapelekea adhabu ya kifo kutokomezwa nchini humo. Mwishoni mwa mwaka 2017 kulikuwa na mataifa 20 ambayo yameachana na adhabu hiyo katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara.

Kwa jumla watu 23 waliuwawa Marekani mwaka jana. Washington ikawa ya ishirini kutokomeza hukumu ya kifo mwezi oktoba mwaka 2018.

Mahakama kuu ya taifa hilo inadhani kuwa adhabu zilikuwa zinatolewa kiupendeleo na bila utaratibu.

Idadi ya nchi ambazo rasmi zimeachana na hukumu ya kifo zinaongezeka kutoka 48 mwaka 1991 mpaka 106 mwaka 2017.

Hivi karibuni, baadhi ya nchi ambazo zimetekeleza hukumu hiyo zimekataa kuhusika.

Anti-death penalty protest outside the Supreme Court in the US.

Chanzo cha picha, AFP

Mataifa ambayo yametekeleza hukumu ya kifo kati ya mwaka 2013 na 2017

Afghanistan, Bahrain, Bangladesh, Belarus, Botswana, Chad, China, Egypt, Equatorial Guinea, India, Indonesia, Iran, Iraq, Japan, Jordan, Kuwait, Malaysia, Nigeria, Korea Kaskazini, Oman, Pakistan, Palestina,

Saudi Arabia, Singapore, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Taiwan, Thailand, United Arab Emirates, USA, Vietnam na Yemen.

(Na kutokana na mgogoro ambao ulikuepo Libya na Syria, Amnesty International haijaweza kuthibitisha kuwa mahakama za mataifa hayo hawakutekeleza adhabu hiyo katika nchi zao).

Nchi 21 ambazo hazijatekeleza hukumu ya kifo katika miaka hiyo licha ya kuwa hazijaachana na adhabu hiyo

Antigua na Barbuda, Bahamas, Barbados, Belize, Comoros, Cuba, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Dominica, Ethiopia, Gambia, Guyana, Jamaica, Lebanon, Lesotho, Qatar,

Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadines, Trinidad na Tobago, Uganda na Zimbabwe.