Khashoggi azidi kuumiza vichwa

Chanzo cha picha, AFP
Nchi za Uingereza,Ujerumani na Ufaransa wametaka kufanyike kwa uchunguzi wa kina juu ya kutoweka kwa mwandishi maarufu wa wa habari wa Saudia Arabia Jamal Khashoggy
Mawaziri hao wa mambo ya nje wamesema kuwa iwapo mtu yoyote atahisiwa kuhusika atawajibika na kuitaka mamlaka ya Riyadhi kutoa taarifa.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jeremy Hunt amesema kuwa haya yote yanayotokea kwa sasa ni juu ya Saudi Arabia ingawa nchi hiyo yenyewe imekanusha kuhusika kutoweka au kuuwawa kwa Khashoggi katika ubalozi wake Instanbul nchini Uturuki
Vyanzo vya habari vilivyonukuliwa na chombo cha habari cha serikali ya Saudia imekanusha kuwa hiyo ni kutokana na sababu za tishio la kisiasa na kiuchumi na watapambana na hatua yoyote itakayochukuliwa dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo.

Khashoggi, aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudia Arabia alitoweka tangu octoba 02 baada ya kuingia katika ubalozi wa nchi hiyo Instambuli nchini Uturuki.
Kwa pamoja mawaziri hao wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu za ulaya wametaka uchunguzi wa kina ufanyike ili wale wote waliohusika kuwajibishwa na taarifa za ukweli wa kilichotokea kwa Khashoggi kijulikane hadharani.
Donald Trump anasema kuwa ni jambo la kutia hasira iwapo kama Saudi Arabia imehusika na kutoa maagizo ya mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi
Tukio hilo huenda likamuweka pabaya mwana mfalme wa Saudia Mohamed bin Salman kutokana na kueneza agenda yake mabadiliko baada ya wafadhili na vyombo vya habari kuamua kujitoa.
Saudi Arabia imejibu vikali kutokana na kunukuliwa kwa chombo chake cha habari SPA kikisema kuwa Utawala wa kifalme iko tayari kukubaliana na vikwazo vya aina yoyote vya kiuchumi au shinikizo la kisiasa

Chanzo cha picha, AFP
Lakini Jumapili jioni Mfalme Salman alijitokeza hadharani akimuunga mkono na kumshukuru rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa kuunda tume ya pamoja itakayofanya uchunguzi wa kutoweka kwa mwandishi huyo, na kusema kuwa hakuna wa kuuvuruga uhusiano wake na nchi hiyo.
Vyanzo vya usalama vya Uturuki vimeimbaia BBC kuwa vina ushahidi wa sauti na video kuwa Khashoggi, ambaye alikuwa akiliandikia gazeti la Marekani la Washington Post, ameuwawa na kundi la watu 15 ndani ya ubalozi wa Saudia Arabia nchini Uturuki alipoingia kwa ajili ya kuomba kibali kwa ajili ya kufunga ndoa.
Jamal Khashoggi ni nani?
- Bwana Khashoggi ni mwandishi wa habari mashuhuri ambaye amewahi kuangazia, taarifa za jinsi Sovieti ilivyovamia Afghanistan na kuibuka kwa Osama Bin Laden.
- Amefanya kazi katika mashirika kadhaa ya habari nchini Saudi Arabia.
- Aliwahi kuwa afisaa wa ngazi ya juu wa Saudi Arabia, lakini baadaye akatofautiana na serikali.
- Mwaka jana alikimbilia uhamishoni nchini Marekani ambako amekuwa akiandika makala ya kila mwezi katika gazeti la Washington Post.
- Katika makala yake ya kwanza ya gazeti hilo, Bw Khashoggi alisema kuwa anagopa kukamatwa kwa kukosoa wazi wazi utawala wa nchini Saudi Arabia.
- Siku tatu kabla ya kutoweka kwake Khashoggi, aliambia BBC kuwa "Watu wanao kamatwa si wapinzani wa serikali na kwamba wana uhuru wa kujielezabali wanajieleza.

Chanzo cha picha, AFP/GETTY IMAGES
Matukio kuelekea kutekwa kwa Khashoggi Oktoba 2
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Uturuki:
03:28: Ndege ya kwanza ya kibinafsi iliyokuwa imebeba maagenti wanaoshukiwa kuwa wa Saudia iliwasili uwanja wa ndege wa Istanbul.
05:05: Maajenti hao walichukua chumba cha malazi katika hoteli moja karibu na jengo la ubalozi .
12:13: Magari kadhaa ya kidiplomasia yanayodaiwa kuwabeba baadhi ya maagenti hao yanaswa katika video yakiwasili ubalozi huo wa Saudia
13:14: Bwana Khashoggi anaonekana akiingia jengo la ubalozi.
15:08: Magari ya yanaondoka jengo la ubalozi yanachukuliwa video yakiwasilia makaazi ya balozi karibu na hapo.
17:15: Ndege ya pili iliyobeba maafisa wanaoshukiwa kuwa wa Saudi Arabia inatua Istanbul.
17:33: Mchumba wa Khashoggi, Hatice Cengiz, anaonekana katika picha za CCTV akisubiri nje ya ubalozi.
18:20: Moja y andege ya kibinafsi anaondoka uwanja wa ndege wa Istanbul.
21:00: Ndio muda ambao ndege ya pili iliondoka.














