Kutoweka kwa Jamal Khashoggi :Saudi Arabia yakataa kupokea vitisho vya kisiasa na kiuchumi

Saudi Arabia imekataa kupokea "vitisho vya kisiasa na kiuchumi" juu ya kupotea kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, idara ya habari ya Saudi Arabia imeharifu.
Taifa hilo limeeleza kuwa linaweza kujibu shinikizo lolote kwa kuchukua hatua kubwa zaidi,mmoja wa maafisa wa juu ambaye jina lake alifahamiki alisema."
Khashoggi, ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia alitoweka Oktoba 2 katika mazingira ya kutatanisha baada ya kutembelea ubalozi wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki.
Rais wa Marekani Donald Trump alidai kuiadhibu Saudi Arabia kama itabainika kuwa nchi hiyo imehusika kumuua mwandishi huyo.
Aidha mamlaka ya Istanbul inaamini kwamba Khashoggi aliuawa alipokuwa anajadiliana na watu kutoka Saudi Arabia hivyo kukataa malalamiko hayo ni uongo.
Kupotea kwa mwandishi huyo kumepelekea Uingereza na Marekani kukataa kuhudhuria mikutano mikubwa ya kimataifa iliyofanyika Saudi Arabia mwezi huu.
Uchumi wa Saudi Arabia una ushawishi mkubwa duniani

Saudia Arabia ambayo imekuwa na shinikizo kubwa la kimataifa juu ya kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari imejibu kukataa kupokea vitisho vyovyote ambavyo vinatokana na msukumo wa kisiasa au kiuchumi.
Nchi hiyo imedai kujibu hatua yeyote itakayochukuliwa kwa kuchukua hatua kubwa zaidi.
Mwanadiplomasia James Landale ameiambia BBC kuwa Katibu wa Hazina wa Marekani Steve Mnuchin na Katibu wa Biashara wa Kimataifa wa Uingereza Liam Fox wamekataa kuhudhuria mkutano mkuu wa uwekezaji ambao utafanyika mwezi ujao huko Riyadh, unajulikana kama "Davos in the desert".

Chanzo cha picha, AFP
Tukio hilo ambalo limeandaliwa na mwana wa mfalme Mohamed bin Salman kwa lengo la kuhamasisha ajenda ya marekebisho. Wadhamini kadhaa na vyombo vya habari wameamua kujitoa .
Taarifa inayothibitisha kwamba bwana Khashoggi aliuawa na watu kutoka Saudi inajadiliwa na wanadiplomasia wa Marekani na Ulaya.
Rais Trump alisema nini kuhusu kutoweka kwa Jamal Khashoggi

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais Donald Trump wa Marekani alihaidi kuiadhibu Saudi Arabia na kama hawataadhibiwa na Marekani basi Urusi au China itawaadhibu.
"Hatuwezi vumilia vitendo kama hivyo kutokea kwa waandishi ama kwa mtu awaye," Trump.
Jamal Khashoggi ni nani?
Khashoggi ni mwandishi wa habari mashuhuri ambaye amewahi kuangazia, taarifa za jinsi Sovieti ilivyovamia Afghanistan na kuibuka kwa Osama Bin Laden.
Amefanya kazi katika mashirika kadhaa ya habari nchini Saudi Arabia.
Aliwahi kuwa afisaa wa ngazi ya juu wa Saudi Arabia, lakini baadaye akatofautiana na serikali.
Mwaka jana alikimbilia uhamishoni nchini Marekani ambako amekuwa akiandika makala ya kila mwezi katika gazeti la Washington Post.
Katika makala yake ya kwanza ya gazeti hilo, Bw Khashoggi alisema kuwa anagopa kukamatwa kwa kukosoa wazi wazi utawala wa nchini Saudi Arabia.
Siku tatu kabla ya kutoweka kwake Khashoggi, aliambia BBC kuwa "Watu wanao kamatwa si wapinzani wa serikali na kwamba wana uhuru wa kujielezabali wanajieleza.












