Kwa Picha: Melania Trump alivyozuru mbuga ya wanyama

Hii ni mara ya pili kwa wake hao wa viongozi kukutana, kwani mara ya kwanza walikutana Ikulu ya White House mjini Washington DC wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais Kenyatta mwezi Agosti mwaka huu.

Mke wa Rais wa Marekani, Melania pamoja na mke wa rais wa Kenya Magret Kenyatta

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mke wa Rais wa Marekani, Melania pamoja na mke wa rais wa Kenya Margaret Kenyatta katika mbuga ya wanayama ya Nairobi.

Ajenda ya ziara ya Bi. Trump inawiana na harakati za shirika la Beyond Zero la Bi Kenyatta ambazo hushughulikia maslahi ya akina mama wajawazito, watoto wachanga, vijana waliobalehe, miongoni mwa masuala mengine mengi ya afya.

Mke wa rais wa Marekani Melania Trump na mmoja wa maafisa wake katika mbuga ya kitaifa ya wanyama nchini Kenya.

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha, Mke wa rais wa Marekani Melania Trump na mmoja wa maafisa wake katika mbuga ya kitaifa ya wanyama nchini Kenya.

Kabla ya kusafiri kuja nchini Kenya, Bi Melania Trump alianza ziara yake katika bara hili huko nchini Ghana mapema wiki hii kabla ya kwenda Malawi.

ndani ya mbuga ya wanyama Kenya
Maelezo ya picha, Tembo wakilishwa katika mbuga ya wanyama

Bi. Trump na mwenyeji wake Mkewe Rais Kenyatta pia watatafuta jinsi watakavyoimarisha ufungamano kati ya mashirika yao ambayo yanashughulikia masuala ya afya ya kina mama na watoto wachanga.

Mke wa Rais wa Marekani, Melania pamoja na mke wa rais wa Kenya Margaret Kenyatta wakiwa na maafisa wa mbuga ya wanayama ya Nairobi.
Maelezo ya picha, Mke wa Rais wa Marekani, Melania pamoja na mke wa rais wa Kenya Margaret Kenyatta wakiwa na maafisa wa mbuga ya wanayama ya Nairobi.

Mke wa Rais wa Kenya,Margaret Kenyatta akiwa ziarani na mke wa rais wa Marekani Melania katika mbuga ya wanyama nchini Kenya

Mke wa rais Kenyatta Margaret Kenyatta
Maelezo ya picha, Mke wa rais Kenyatta Margaret Kenyatta akiwa katika mbuga ya kitaifa ya wanyama nchini Kenya

Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump na mke wa Rais wa Kenya Margaret Kenyatta walitembelea kituo cha wakfu wa kuhifadhi wanyama pori cha David Sheldrick.

Tembo
Maelezo ya picha, Tembo

Ziara ya Bi Melania Trump nchini Kenya inafuatia mashauriano waliyofanya na Mkewe Rais Margaret Kenyatta katika Ikulu ya White House wakati Mama wa Taifa aliandamana na Rais Uhuru Kenyatta katika ziara ya mwezi Agosti mwaka huu huko mjini Washington DC.

Melania Trump na Margaret Kenyatta

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Melania Trump na Margaret Kenyatta wakimpapasa ndama wa tembo

Bi Trump atatamatisha ziara yake ya bara Afrika kwa kuzuru Misri.

Atazingatia zaidi huduma za afya kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, elimu na jukumu linalotekelezwa na Marekani Kenya kujitosheleza katika utoaji huduma.

Hii ni mara ya pili kwa wake hao wa viongozi kukutana, kwani mara ya kwanza walikutana Ikulu ya White House mjini Washington DC wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais Kenyatta mwezi Agosti mwaka huu.