Takribani wahamiaji 60 wanahofiwa kufa maji baada ya boti kupinduka Guinea Bissau

Boti iliyozama ilifanana na hii ya Dakar, Senegal
Maelezo ya picha, Boti iliyozama ilifanana na hii ya Dakar, Senegal

Takribani wahamiaji 60 wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliokua wakisafiria kupigwa na dhroruba na kupinduka huko Guinea Bissau. Vikosi vya majini vimeshindwa kuwasaidia baada ya boti hiyo kuzama siku ya jumatatu kufuatiwa na ukosefu wa vifaa vya kuokolea.

Mkuu wa mamlaka ya bandari wa taifa aliiambia BBC , baadhi ya mabaki ya boti hiyo yamepatikana lakini hakuna miili iliyoweza kutambulika.

Haijajulikana ni wapi boti hiyo ilipokua inaelekea lakini ilikua ikikatisha kisiwa cha Kanari huko Uhispania ambapo ni kilomita 1,120 kutoka Guinea Bissau.

Picha ya satelite ikionyesha sehemu ilipozama meli hiyo

Hata hivyo njia hiyo imepungua kutumiwa na wahamiaji tangu walipoongeza kufanya doria katika bahari ya Atlantic miaka ya tisini. Ajali nyingi za majini za wahamiaji zinasabishwa na kujaa watu na mizigo huku Afrika ya kati ikihusishwa.

Kufuatia mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi na kushindwa kufanya uzalishaji, Guinea Bissau ni moja ya nchi maskini kabisa duniani.

Maelezo ya video, Tazama maandalizi ya kuitoa MV Nyerere kwenye maji

Nchi hii imekua na deni kubwa na uchumi unategemea zaidi kwenye misaada ya nje na imefanya kutumia zaidi usafiri wa meli kusafirishia madawa kuelekea Amerika ya Kusini miaka ya hivi karibuni.

Wengi wao ni vijana amabao wanashindwa kupata kazi na kuamua kwenda nchi za nje kutafuta maisha bora.