Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mtalii auawa kwa kunyagwa na tembo alipojaribu kumpiga picha Zimbabwe
Mtalii wa Ujerumani amefariki baada kukanyagwa na tembo alipokuwa akijaribu kumpiga picha chini Zimbabwe.
Mamlaka nchini humo imethibitisha kuwa mkasa huo ulifanyika katika mbuga ya kitaifa ya Mana Pools na kwamba mwanamke huyo alifariki siku hiyo kutokana na majeraha aliyopata.
Mwanamke ambaye jina lake halijabainika alikua miongoni mwa kundi la watalii waliyokutana na tembo walipoingia katika mbuga ya wanyama.
Visa vya watu kushambuliwa na tembo vimekithiri sana nchini Zimbabwe.
Mara nyingi wanyama hao huvamia mashamba wakulima.
Msemaji wa Mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori nchini Zimbabwe,Tinashe Farawo, amesema mamlaka hiyo haijabainisha chanzo cha shambulio hilo.
"Tunawaomba watu kukaa mbali na wanamapori na kuwa waangalifu wanapokutana nao''.
Katika tukio jingine sawia na hilo mwaka jana, raia wa Zimbabwe aliuawa na tembo alipokua akijaribu kuwaelekeza sehemu ya wazi ili awezi kuwapiga picha
Zimbabwe ni taifa la pili duniani lililo na idadi kubwa ya tembo. Kwa mujibu wa sensa ya tembo ya mwaka 2016 taifa hilo lina tembo elfu 82,304
Mataifa mengine ya Afrka yaliyo na tembo wengi ni yapi?
- Botswana: 130,451
- Zimbabwe: 82,304
- Tanzania: 42,871
- Kenya: 25,959
- Zambia: 21,758