Patrick Mfugale: Mhandisi nchini Tanzania ambaye jina lake limepewa daraja jipya la juu

daraja la muhandisi Patrick Mfugale Tanzania

Patrick Aron Nipilima Mfugale Alizaliwa katika eneo la Ifunda huko Iringa.

-Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa

-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.

-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi

-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India

-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.

-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.

-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, Braunshweig nchini Uingereza

-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.

-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.

-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System

-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.

-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .

Alibuni daraja la Magarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.

-Baadhi ya madaraja alioweza kujenga ni:

  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha tanzania na Moxzambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo huko Mara
  • Daraja la Kikwete huko Magarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni

- Mfugale ambaye kwa sasa ni mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.

Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.

- Ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.

- Ni mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.

-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency