Mkenya Waihiga Mwaura ameshinda tuzo ya BBC ya Komla Dumor

Mwandishi wa habari mkenya na mtangazaji wa televisheni ndiye mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya BBC ya Komla Dumor.
Waihiga Mwaura ni msomaji wa habari za jioni kwenye kituo kinachotazamwa sana Kenya cha Citizen.
Kama sehemu ya tuzo hiyo, kwa miezi mitatu atakuwa kwenye ofisi ya BBC mjini London na baadaye kurudi Afrika kuendelea na kazi.
Tuzo hilo lilibuniwa kwa heshima ya Komla Dumor mtangazaji wa BBC World News, ambaye alikufa ghafla akiwa aa umri wa miaka 41 mwaka 2014.
Bw Mwaura ndiye mshindi wa nne wa tuzo hilo, baada ya tuzo la kwanza kushindwa na Nancy Kacungira mwaka 2015 akifuatiwa na Wa Nigeria Didi Akinyelure na Amina Yuguda.
Ni mwandishi wa habari maarufu nchini Kenya ambaye hutangaza kuhusu masuala tofauti yakiwemo michezo na siasa.
"Komla Dumor alikuwa mtu wa maana sana kwangu kama mwandishi wa habari na kwangu mimi mwennyewe. "Kama nitafanikiwa kwa asilimia 10 au 20, ya kile nifanya nitahisi nitakuwa nimetoa mchango sana kwa uandishi wa habari.
Aliridhisha jopo la majaji kutokana na uwezo wake wa kuripoti.





-resize.jpg.webp)








