Maandamano ya kupinga vita vya kikabila yafanyika Addis Ababa Ethiopia

Waandamanaji wenye hasira kali wameuzingira mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa baada ya kuuawa kwa watu 23 wakati wa mapigano ya kikabila yaliyoibuka mwishoni mwa juma lililopita.
Wamezuia barabara kuu za jiji hilo, sambamba na kufunga biashara mbalimbali wakiitaka serikali ichukue hatua muhimu kuzuia mauaji hayo.
Wakaazi wa jiji hilo wanawalaumu vijana wa kabila la Oromo kuwa walianzisha fujo katika mitaa ya mji wa Burayu ambapo walitumia visu, mawe na vyuma.
Polisi inasema zaidi ya watu 200 wamekamatwa kufuatia mapigano hayo.
Migogoro ya kikabila imeogezeka nchini Ethiopia tokea waziri mkuu anayetajwa kuleta mageuzi makubwa nchini humo Abiy Ahmed Ali kuingia madarakani mwezi April.








