Ni kwa jinsi gani ugonjwa wa ndui ulitokomezwa duniani?

Ndui (smallpox) ulikuwa ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na virusi aina ya variola.Ugonjwa huu ulikuwa unasababisha vifo kwa asilimia 30 mpaka 35, walioathirika zaidi walikuwa ni watoto.

Huku walionusurika wengi waliachwa na makovu ya kudumu hasa katika uso.

Mwaka 1978 ,mgonjwa wa mwisho wa ndui aliripotiwa nchini Uingereza.Lakini ni namna gani ugonjwa huu ulidhaniwa kuwa umetokomezwa duniani kote uliweza kuibuka tena katika mji mkubwa wa pili wa Uingereza?

Bibi harusi mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikuwa ni mpiga pichaJaneth Parker aliananza kutojisikia vizuri siku ya ijumaa tarehe 11 agosti.

Ndani ya siku chache bi.Parker,aliyekuwa anafanya kazi katika chuo cha ya afya Birmingham alianza kupata madoa yenye rangi nyekundu katika mgongo wake na usoni.

Alipoenda kumuona daktari aliambiwa ana tetekuwanga (chickenpox) na majibu hayo yalikuja kwa sababu mwaka huo 1978 dunia ilikuwa imeshatangaza kutoweka kwa ugonjwa wa ndui.

Lakini mama yake bi Parker , Hilda Witcomb alikuwa na mashaka na majibu hayo kwa sababu vipele ambavyo mwanae alikuwa anavipata vilikuwa vina utofauti mkubwa na vile ambavyo watu wanakuwa navyo wanapougua tetekuwanga.

Agosti 20,bado hali ya bi.Parker haikuwa na nafuu yeyote na alikuwa dhaifu sana ,alishindwa hata kusimama mwenyewe.

Prof Symmons ndiye aliyemfanyia uchunguzi bi.Parker,na hofu ya madaktari ikarudi tena pale alipobainika kuwa na virusi vya "variola" .

Ndui iliyokuwa imetangazwa kutoweka duniani kote baada ya kesi ya mgonjwa wa mwisho kuripotiwa nchini Somalia mwaka 1977 imerudi katika mji wa Birmingham nchini Uingereza.

Ugonjwa huo uliowahi kuepo kwa miaka mingi ulikuwa unaogopwa duniani kote

Katika karne ya 20 tu ilikadiriwa kuwa watu zaidi ya milioni 300 walikufa kutokana na ugonjwa huo.

Wale ambao waliugua ndui na kupona wengi wao walibaki na makovu mabaya.

Mpango wa chanjo duniani kote ulioongozwa na shirika la afya duniani (WHO), ulifanyika ili kutokomeza ugonjwa wa surua na ilipofika mwaka 1970 kesi za ugonjwa huo zilikuwa chache.

Na ilipofika mwaka 1978 ,shirika hilo la afya lilitangaza kutokuwepo kwa ugonjwa huo tena duniani kote .

Sehemu ambayo hakuna mtu alidhania kuwa ugonjwa huo unaweza kulipuka tena ilikuwa ni Uingereza kwa sababu hakukuripotiwa mgonjwa yeyote wan dui kwa kipindi cha miaka mitano mpaka bi.Parker alipotangazwa.

Matokeo ya kurejea kwa ugonjwa huo ulishangaza ulimwengu wote na kuleta hofu mpya.