Suala la Brigitte Nielsen kupata mtoto akiwa na miaka 54 limeibua mjadala

Chanzo cha picha, Getty Images
Taarifa kwamba Brigitte Nielsen amejifungua mtoto akiwa na umri wa miaka 54 imeibua hisia zaidi kuhusu kuongezeka kwa idadi kubwa ya akina mama wanaopata watoto wakiwa na umri mkubwa.
Brigitte -mchezaji filmu ambae alijifungua mtoto wa kike Frida mwezi Juni, alijipata akilazimika kutetea uamuzi wake wa kupata mtoto baada ya kukosolewa.
"Baadhi ya wanawake hufikiria , 'Oh Mungu wangu , Mimi nina umri mkubwa sana,' Lakini hawajiulizi ni wanaume wangapi wanaopata watoto wao wa kwanza wakiwa na umri wa miaka 60 na 70 na hawakuwahi kuwa na wasi wasi wowote juu ya hilo?.
"Ninakubali kabisa kwamba si kila mtu anapenda hili, lakini ni maisha yangu, na mume wangu na nina uhusiano thabiti ," Aliliambia jarida la People.
Nielsen aliolewa na Mattia Dessi, ambae ana umri wa miaka 39, mwaka 2006, na akaanza kuhifadhi mayai yake ya uzazi kwenye friji akiwa na umri wa miaka 40.
Anasema aliambiwa kuwa ana uwezo wa asilimia 3-4 % wa uwezo wa kupata ujauzito kwa kutumia mayai yake ya uzazi, na ameweza kufanikiwa baada ya kutumia njia ya kusaidiwa kutunga mimba IVF kwa mika 14.
Frida ni mtoto wake wa kwanza na Dessi, licha ya kwamba muigizaji filamu huyo wa Denmark anawatoto wengine 4 aliowapata kwenye ndoa za kwanza .
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Uzazi baada ya kipindi cha uzazi (Post-menopausal Motherhood)
Idadi ya akinamama wanaojifungua wakiwa na umri mkubwa imeongezeka, huku viwango vya uwezo wa kupata ujauzito kwa wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 40 vikiongezeka mara dufu tangu mwaka 1990.
Takwimu zilizotolewa mwaka huu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (ONS) zinaonesha kuwa viwango vya kupata ujauzito mwaka 2016, vilipungua katika makundi mbali mbali ya umr, isipokuwa kwa wanawake wenye umri wa miaka 40 na zaidi ambapo viwango viliongezeka kwa 2%.

Chanzo cha picha, Getty Images
Takwimu hizo kwa sasa haziwatengi wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 50, lakini wataalam katika kliniki za uzazi wanasema idadi ya wanawake wanaotafuta tiba ya uzazi wenye umri wa miaka zaidi ya 40 na 50 inaongezeka.
Dkt. Janine Elson, Mkurugenzi wa vituo vya huduma za klinic za uzazi wa kusaidiwa kwa njia ya IVF, anasema kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wanawake wanaotaka kupata ujauzito wenye umri wa zaidi ya miaka 50 na kwa sasa wameandaa vijikaratasi vya maelezo rasmi kwa ajili ya wanawake hao.
Athari za kupata ujauzito katika umri mkubwa:
Licha ya kwamba wanawake wengi wameweza kuwapata watoto wenye afya nzuri wakiwa na umri mkubwa, wataalam wanasisistiza kwamba:
- Wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 50 mara nyingi watalazimika kupokea msaada wa mayai ya uzazi, ikiwa hawakuyatunza awali kwenye friji wakiwa na umri mdogo
- Watalazimika kufanyiwa uchunguzi wa kina kwasababu wanakuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari, ongezeko na mafuta mwilini na saratani ya matiti
- yeyeto anayejifungua akiwa na miaka zaidi ya 35 na zaidi anakabiliwa na hatari kubwa ya kupata kisukari, na kiharusi .
- Ikiwa watatumia mayai yao binafsi ya uzazi, hatari ya kupata kasoro za urithi huongezeka zaidi kadri umri unavyoongezeka
- Wanawake wenye umri wa kuanzia miaka wanaweza pia kupata changamoto ya kunyonyesha watoto kutokana na matatizo matatizo ya kiafya yanayowapata wanawake wanaopitia kipindi cha baada ya uzazi (menopouse)
- Kukosa msaada kutoka kwa marafiki kutokana na uchache wa wanawake wanaojifungua wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 40 na 50.
- Na kama alivyosema Brigitte Nielsen mwenyewe jamii humkaripia mwanamke anayepata umri mtoto akiwa na umri mkubwa kinyume na mwanamume mwenye umri sawa.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Hakuna mtu yeyote aliyekasirishwa na kitendo cha George Clooney kuwa baba akiwa wa mapacha akiwa na umri wa miaka 56.
Inapokuja katika suala la kuwa baba, tunahisi kwamba hawapaswi kuguswa.
"Wanawake kwa upande mwingine wanashutumiwa kwa kuwa wabinafsi kwa kuchelewa sana kuwa wamama ." Alisisitiza Brigitte Nielsen.
Kliniki ya Wanawake ya London hutoa matibabu ya wanawake kwa kutoa msaada wa mayai ya uzazi kwa wanawake hadi wa umri wa miaka 54.
Kliniki hiyo pia imeshuhudia ongezeko kubwa la wanawake wanaokuja kuhifadhi mnayai yao ya uzazi kwenye friji kati ya mwaka 2004na 2015.
Katika kituo cha taifa cha afya ya uzazi huduma ya matibabu ya uzazi wa kusaidiwa - IVF hutegemea mambo mbali mbalii kulingana na eneo lako, na mwongozo wa sasa unapendekeza msaada utolewe tu kwa wanawake walio na umri hadi wa miaka 42.












