Mwita Waitara: Mbunge wa Chadema ajiunga na CCM Tanzania

Mbunge wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania Mwita Waitara

Chanzo cha picha, Mwita Waitara/Facebook

Muda wa kusoma: Dakika 1

Mbunge wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania Mwita Waitara amejiunga na chama tawala nchini humo CCM.

Waitara kutoka eneo bunge la Ukonga alitangaza uamuzi huo katika mkutano na vyombo vya habari mapema Jumamosi.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Katika mkutano huo ulioandaliwa na katibu wa CCM anayesimamia maswala ya umma Humphery Polepole, kiongozi huyo amesema kuwa ameamua kurudi katika chama tawala ili kumsaidia rais John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kuleta ukuwaji wa uchumi na maendeleo nchini humo.

''Ilikuwa vigumu kwangu mimi kama mbunge wa upinzani kusimamia miradi ya maendeleo katika eneo bunge langu kwa sababu nilizuiwa na maafisa wakuu wa Chadema hata kufanya mkutano na mawaziri'', alisema.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Aliongezea: kuna maswala ambayo nililazimika kukubaliana nayo licha ya kwamba hayakuwapendeza wakaazi wa eneo bunge langu. Nimeamua kuhamia CCM kwa ajili ya wapiga kura wa eneo bunge langu.

"Mimi nataka kufanya kazi nataka niende mahali ambapo kuna kazi za kufanya, nitoe wito kuna vijana wanaangalia kutoka Tarime kwenda

Kakonko mimi ni ndugu yao niwaambie wasitumike watu wana mipango yao," alinukuliwa na gazeti la mwananchi akisema.

Waitara amesema sababu watumishi wa umma wamekuwa na nidhamu tangu awamu ya tano ilipoingia madarakani.

"Kuna mabadiliko makubwa na sekretarieti imebadilika, Mwenyekiti wa chama ni mwingine, watendaji na mawaziri spidi ni kubwa, wanatoa

majibu kwa wananchi na watu wanasikilizwa," amesema.