Kwa Picha: Mwezi mwekundu ulivyoonekana kote duniani
Watu katika mataifa mengi dunia walifanikiwa kutaza kupatwa kwa mwezi uliobadilika na kuwa mwekundu ikiwa ni tukio la muda mrefu la aina yake katika karne ya 21.

Chanzo cha picha, Reuters
Nchini Ugiriki, mwezi ulipanda nyuma ya hekalu la Poseidon mjini Cape Sounion, karibu na mji mkuu wa Athens.
Katika tukio la kupatwa kwa mwezi, dunia kuwa katikati ya mwezi na jua

Chanzo cha picha, Getty Images
Ijapokuwa hupata mwangaza moja kwa moja kutoka kwa Jua, mwezi huo ulikuwa ukipata mwanga kidogo unaotokana na kuinama kwa mbingu ya dunia.
Hatua hiyo unaipatia mwezi huo rangi ya machungwa, kahawa au nyekundu.
Mwezi huo ulionekana kutoka Afrika hadi Mashariki ya Kati, Ulaya, Urusi, India na Australia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mjini Strasbourg, Ufaransa, mwezi ulionekana ukipitia juu ya sanamu hii iliochongwa na msanii wa Marekani Jonathan Borofsky.

Chanzo cha picha, EPA
Nchini Uswizi uliweza kuonekana juu ya kilele cha milima ya Alps

Chanzo cha picha, Reuters
Watu waliokuwa wakiutizama hawakuhitaji kifaa chochote ili kuuona mwezi huo.

Chanzo cha picha, Reuters
Huku mwezi huo iukipita juu ya Abu Dhabi, uliweza kuonekana katika mnara mrefu mwembamba wa msikiti mkubwa wa Sheikh Zayed .

Chanzo cha picha, Getty Images
Mjini Sydney, umati wa watu ulikusanyika ili kutazama Mwezi mwekundu katika u juu ya mbingu todauti za mji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu huko Taipei, Taiwan, walianzisha vifaa vya teknolojia ili kutazama tukio hilo. kupatwa kwa mwezi kulichukua takriban saa moja na dakika 43.












